Mwigizaji anayechipukia, Mariam Ismail amesema umaarufu wa
msanii hauji kwa kuandikwa vibaya na vyombo vya habari, bali ni kutokana
na sifa alizonazo katika kazi yake ya sanaa.
“Umaarufu wa msanii si lazima ajengwe kwa
kuandikwa kashfa katika vyombo vya habari bali ni kuitendea haki filamu
anayochaguliwa.”
Mariam anaamini anafanya hivyo katika filamu
anazocheza kila anapochaguliwa jambo ambalo hivi sasa kila mtayarishaji
anahitaji kufanya naye kazi kwa sababu anajua.
Alisema wasanii wengi hasa wa filamu wamekuwa na
tabia ya kutengeneza kashfa na wakati mwingine kuvaa nusu uchi ili tu
watokeze kwenye vyombo vya habari jambo ambalo linawashushia heshima
katika jamii.
“Wasanii tumekuwa na tabia ya kutokujijali, watu
wanavaa nusu uchi na malengo yao hasa ni kutokea kwenye vyombo vya
habari,” alisema Mariam. Na Herieth Makwetta
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni