KIWANDA CHA KUSAFISHIA MADINI YA DHAHABU KINACHO KILICHOPO GOMBE KUSINI MKOANI MBEYA KIKIMILIKIWA NA STEWART MWITA KIMEIBUA JIPYA
wananchi wa Gombe kusini mkoani Mbeya wamelalamikia uwepo wa kiwanda cha kusafishia madini ya dhahabu kinachomilikiwa na Stewart Mwita wakidai kuwa kimekuwa kikitiririsha moshi na kusababisha harufu kali ambayo walisema ni kero na hatari kwa afya za wananchi wa eneo hilo.
Wakizungumza na Baragumu wananchi hao walisema kuwa, kiwanda hicho kinatoa sumu ambayo ina madhara makubwa kwa watu wa eneo hilo ikiwemo kukohoa mara kwa mara.
Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Godfrei Kapunga alisema kuwa taarifa walizitoa katika ofisi ya Mkoa na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya kiwanda hicho.
Akizungumzia suala hilo Afisa wa madini Mkoa wa Mbeya, alisema kuwa madhara yanayo sababishwa na utiririshwaji wa maji taka kutoka katika kiwanda hicho yanaweza kusababisha madhara hasi kwa wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho ambacho wanaathirika na maji hayo taka yenye kemikali kama vile mekyuri ambazo zinaweza kuwa hatari kwa binadamu.
Afisa madini alisema kiwanda hicho kinapaswa kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira au la uongozi wa Mkoa utalazimika kukiondoa katika eneo hilo iwapo itabainika kimejengwa jirani na makazi ya watu.
Wakitoa maoni yao wananchi wa mtaa wa Gombe kusini walisema kuwa wanaomba kiwanda hicho kiondolewe maramoja, pia wanaomba kupimwa afya zao na kwamba iwapo watabainika kupata madhara kutokana na taka za kiwanda hicho basi watadai fidia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni