Ni wengi wanaoutumia na kuufahamu mchaichai kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu.
Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana faida
kubwa kiafya . Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda
vinavyotengeneza pafyumu na sabuni.
Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai una
vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha
tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Watu wengine huamini kuwa
mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo,
matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye
uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.
Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza
kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa
wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na:
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila
gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa
kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya
watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una
uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa
mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya
tumbo ikiwamo kujaa gesi.
Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini.
Na Maimuna Kubegeya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni