KATIBU MKUU WA CHAMA CHA SOKA MKOANI MBEYA (MREFA) HAROUB SULEIMANI AKANUSHA MADAI
Timu ya soka ya mkoa wa Mara Polisi jamii bunda ambayo
inashiriki michuano ya mabingwa wa mikoa nchini imewasirisha rufaa kwenye shirikisho la soka nchini TFF Julai 3, mwaka huu.
Polisi bunda kupitia chama cha soka mkoani Mara walituma
malalamiko yanayo ishutumu timu ya kimondo fc ya mkoani Mbeya kwa kupanga
mchezo wao wa marudiano kufanyika siku ya jumamosi badala ya jumapili kama
shirikisho la soka nchini lililivyo amuru kuwa machezo yote ifanyike juni 30
siku ya jumapili.
Aidha akiongea Baragumu katibu mkuu wa chama cha
soka mkoani Mbeya (MREFA) Haroub Suleiman amekanusha madai hayo kwa kusema kuwa
shirikisho la soka nchini limezipa uhuru timu wenyeji katika michuano hiyo
kuamua siku hususa ya mchezo kati ya siku mbili za miisho juma ili kucheza
michzo yake.
Pia Haroub alisema kuwa aliwasiliana na viongozi wa timu ya
Polisi bunda na kuwajulisha siku ya mchezo wao dhidi ya kimondo kuwa ni
jumamosi na ndio sababu walicheza siku hiyo bila kipingamizi, katika mchezo huo kimondo iliibugiza timu hiyo ya
Polisi bunda kwa magoli (3-1)katika uwanja wa kumbu kumbu ya sokoine jijini
hapa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni