Jumanne, 26 Mei 2015

MATOKEO YA BALEHE NI HAYA NA ELIMU YA JINSIA SOMA HAPA


Kuna mabadiliko ya kimwili ambayo hutokea wakati wa kubalehe. Mabadiliko haya ni pamoja na ukuaji na utanukaji wa viungo vya uzazi au jinsia. Wanaume na wanawake wana viungo vya uzazi ambavyo vinaweza kuonekana nje ya miili yao. Wanawake pia wana viungo vya sehemu za siri ndani ya mwili. Viungo hivyo vyote vilivyopo ndani ya mwili huitwa viungo vya ndani ya uzazi na vile vilivyopo nje huitwa ni sehemu za siri.
Viungo vya uzazi vya kike:
Wanawake  wana  njia tatu ndogo katikati ya miguu yao. Mbele kuna njia  iitwayo urethral  ambayo huitumia kwa ajili ya haja ndogo. Njia ya haja kubwa (anus) ambayo ipo nyuma ambayo huitumia kwa ajili ya kwenda haja kubwa na katikati  kuna mlango ambao unaingia  katika viungo vya ndani vya sehemu ya uzazi (Vagina).Wakati mwanamke anapokuwa katika siku zake  damu hutoka nje kwa njia  hiyo ya katikati. 
Ndani ya uke  kuna  ngozi nyembamba iitwayo hymen. Hymen sehemu ya  kazi yake ni kuzuia  uke, lakini bado  kunakuwepo na nafasi ya kutosha ili kuweza damu  kupita.
Kiungo kingine muhimu ni kisimi au kinembe (clitoris). Hiki kina ukubwa wa kila aina na kipo mbele ya kiungo cha nje cha uke wa  mwanamke.  Kiungo hiki ni chombo nyeti sana sawa na viungo vingine nyeti kwa mwanamme na husaidia mwanamke kujisikia furaha wakati wakiburudishana na mumewe. Midomo ya nje ya viungo vya mwanamke (labia)  pamoja na kisimi na uwazi wa uke inajulikana kama uke.
Viungo vya uzazi vya kiume:
Kwa upande wa mwanamume, viungo vya nje vya uzazi  ni uume na vifuko viwili (korodani) ambavyo  vinaweza kuitwa kiwanda  cha kuzalisha mbegu za kiume ingawa  kwa lugha ya kitaalamu vinaitwa “pair of testes” (ama wakati mwingine uitwa  testicles) Vifuko hivi viwili vipo chini ya kibofu na vimefungwa pamoja kama mfano wa pochi ambao kwa lugha pia ya kitaalamu unajulukana kama ‘scrotum ama scrotal sac’.
Uume ni  chombo ambacho kinaruhusu kupenya ndani ya uke. Uume unaundwa na misuli myembamba sana (tissue spongy) .
Wakati misuli hiyo inapokuwa imejaa sambamba na damu uume unakuwa imara. Wakati kunapokuwa hakuna tendo la ndoa uume upoteza uimara wake  na  damu ya ziada huenda kutumika kwenye viungo vingine vya mwili  na uume unakuwa umesinyaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni