Baada ya wanaume kushindwa kuwaridhisha wapezi wao kunanjia mbadala iliyopendekezwa
Wanaume katika eneo la Meru mashariki mwa Kenya ambao wanasadikiwa kuwa hawana uwezo wa kuwatosheleza wake zao kupitia tendo la ngono sasa wametakiwa kutokuwa na wasiwasi.
Mwakilishi wa wanawake katika eneo hilo Florence kajuju ameanza mpango wa kuwahamasisha wanaume kutumia miraa badala ya ya pombe haramu .
Akizungumza na gazeti la The Nairobian nchini Kenya,kiongozi huyo amesema kuwa pombe haramu hushusha nguvu za kiume na kuwafanya wanaume kushindwa kuwatosheleza wake zao.
”Ni pombe kama hizi ambazo huathiri nguvu za kiume na kusababisha utasa miongoni mwa wanaume”,alisema.
Kajuju ambaye anasema anapenda miraa aliudhika alipogundua kwamba eneo la Meru ni miongoni mwa maeneo ambayo wanaume hawana uwezo wa kutafuta watoto.
”Vijana wetu wameathirika vibaya na pombe haramu na lazima tuwaokoe”.
Alisema kuwa wale waliopiga marufuku uuzaji wa miraa katika mataifa yao wanafaa kugundua umuhimu wa zao hilo miongoni mwa jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni