SEKRETARIETI YA MKOA WA MBEYA YAPENDEKEZA JINA LA MKOA MPYA
Sekretarieti ya mkoa wa Mbeya imependekeza mkoa mpya
utakaoanzishwa uitwe mkoa wa Songwe na makao makuu yake yakiwa Mkwajuni
wilayani Chunya.
Mapendekezo hayo yametolewa julai 4 mwaka huu katika kikao
cha kamati ya ushauri ya mkoa iliyohusisha wajumbe kutoka wilaya zote za mkoa
wa Mbeya iliyofanyika katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya.
Akizungumza kwaniaba ya wajumbe mwenyekiti wa kamati hiyo
ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbasi Kandoro amesema kuwa wamependekeza mkoa
mpya uitwe SONGWE kwa kuzingatia vigezo vilivyo tolewa na ofisi ya waziri mkuu
tawala za mikoa na serikali za mitaa
Aidha Kandoro amesema kuwa mkoa mpya wa Songwe utaundwa na
wilaya za Ileje,Chunya,Mbozi na Momba na makao makuu yake yakiwa ni Mkwajuni
wilayani Chunya wakati mkoa Mbeya utabaki na wilaya za Mbeya,Rungwe,Mbalali na
Kyela.
Hata hivyo wasema kuwa
lengo la kuugawa mkoa ni kutokana na mkoa wa Mbeya kuwa na eneo kubwa hivyo
linastahili kutoa mikoa miwili ili kuboresha huduma kwa wananchi na kuongeza
kasi ya ukuaji wa kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni