CCM YA PATA PIGO
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimeendelea kupata pigo kubwa baada ya kifo cha diwani wa kata ya Nduli, katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Idd Chonanga.
Chonanga alifariki dunia july 3 mwaka huu na kufikisha idadi ya madiwani 8 wa CCM kupoteza maisha kwa kipindi hiki cha miaka mitatu pekee
Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa, Aman Mwamwindi alithibitisha kutokea kwa kifo cha diwani Chonanga na kusema kuwa kifo hicho kilitokea majira ya saa 8 mchana siku ya july 3 katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo diwani huyo alilazwa.
Mwamwindi alisema kuwa Chonanga alifikishwa Hospitalini hapo majira ya saa 12 asubuhi kutokana na tatizo la ugonjwa wa BP ya kushuka, na madaktari walijitahidi kuhangaikia kuokoa maisha yake, lakini ilipofika majira ya saa 8 mchana diwani huyo alifariki dunia.
Hata hivyo Mwamwindi alisema kuwa kifo cha diwani Chonanga ni pigo kubwa ndani ya halmashauri ya manispaa ya Iringa kutokana na utendaji kazi wa diwani huyo katika Halmashauri hiyo kupitia kata yake ya Nduli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni