Jumapili, 21 Julai 2013

SURUALI ZA KUBANA NI HATARI KWA WANAUMESuruali za kubana kwa wanaume ni hatari



 Kwa wananchi wa Uganda, jina la Denzel Mwiyeretsi siyo geni kwa kuwa ni mtangazaji wa masuala ya mjini katika Kituo cha Televisheni cha XFM, lakini Denzel pia ni maarufu kwa wafuatiliaji wa Big Brother kutokana na kushiriki shindano hilo nchini Afrika Kusini. 

 

Hata hivyo, watu wengi wanamfahamu kwa mitindo ya uvaaji wake wa suruali za kubana.

 

“Mitindo ni kama umri, haiwezi kuwa vilevile. Ni kama vile mvinyo mtamu, pamoja na umri, mtindo wako lazima uwe na mwonekano mzuri. Ni kujaribu kitu kipya. Mimi ni mtu mwenye kuthubutu na napenda kujaribu vitu vipya (ikiwamo mitindo) ili kufanya maisha yangu yawe yenye mvuto,” alisema Denzel.

 

Pamoja na tabia yake ya kupenda kuvaa suruali za kubana kuna watu akiwamo dada yake hakupendezwa na hali hiyo, siku moja dada yake alimwambia hapendezwi na uvaaji huo.

 

“Miaka miwili iliyopita, dada yangu aliniambia kuwa uvaaji wangu wa suruali za kubana unaweza kuwafanya watu wanihisi mimi ni ‘shoga’. Lakini nilimueleza uvaaji huo ni mtindo wa maisha yangu,” alisema Denzel aliponukuliwa na gazeti la New Vision la Uganda.

 

Ingawa dada yake anauona uvaaji wake unalingana na wanaume wenye vitendo vya ushoga, aliendelea kutetea kuwa mpenzi wake wa kike amekuwa akimsifia kwa uvaaji wake wa suruali za mtindo wa kubana.

 

Hata hivyo, siyo watu wa kawaida pekee ndiyo wenye kukwazwa na mtindo wa uvaaji wa nguo za kubana wa Denzel. Hata madaktari nao wametoa ushauri wao kuwa uvaaji wa suruali za kubana ni hatari kiafya

.

Lakini hoja za madaktari hazionyeshi kumteteresha Denzel ambaye alijibu kwa kusema kuwa ni madaktari hao hao wanaosema kunywa maji kwa kutumia vyombo vya planstiki ni hatari. Je? tumeacha kunywa maji kwenye chupa za plastiki? Kila tunachofanya ni hatari. Kitu kizuri ni kwamba sijawahi kuugua kwa sababu ya uvaaji wa mtindo wangu wa suruali za kubana.”

 

Mchambuzi wa masuala ya mitindo, Keturah Kamugasa alisema suruali za kubana ni mtindo wa zamani ambao umerudi kwa kasi, hasa kupitia suruali aina ya jinsi. “Zamani zilikuwa zikiitwa ‘bomba’.”

 

Suruali za kubana mwanzoni zilivaliwa na wanasiasa wa kundi la mlengo wa kushoto la Sans-culottes, ambao walikuwa wapinzani wakubwa wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa, wakati huo suruali hizo waliziita ‘pantaloons’.

 

Uvaaji huo ulianza kama uasi na kuwa mtindo wenye umaarufu katika miaka ya 1950. Suruali hizo baadaye zikaanza kuvaliwa na mastaa wa rock’n’roll katika miaka ya 1960 na kuendelea kusambaa katika jamii.

 

Ijumaa, 19 Julai 2013

FAIDA ZA MCHAI CHAI KWA BINADAMU.



Ni wengi wanaoutumia na kuufahamu mchaichai kama kiungo  cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu.

 

Lakini, je unafahamu kuwa majani haya yana faida kubwa kiafya . Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda vinavyotengeneza pafyumu na sabuni.

 

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai una vichocheo  muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Watu wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile  homa ya matumbo, matatizo ya ngozi,  madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.

 

Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na:

 

Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka  Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.

 

Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini. 

Na Maimuna Kubegeya

MKOPO UNAMAMBO YAKE TAZAMA PICHA



Vifaa vya Ofisini mali kampuni ya Scandinavia Express vikiwa vimetolewa nje jijini Dar es Salaam jana. Vilitolewa na madalali wa mahakama kwa madai ya kushindwa kulipa mkopo ambao hata hivyo haikufahamika ni kiasi gani. Picha na Fidelis Felix 

Vifaa vya Ofisini mali kampuni ya Scandinavia Express vikiwa vimetolewa nje jijini Dar es Salaam jana. Vilitolewa na madalali wa mahakama kwa madai ya kushindwa kulipa mkopo ambao hata hivyo haikufahamika ni kiasi gani. Picha na Fidelis Felix

UPEPO WAEZUA NYUMBA



Mkazi wa Mtaa wa Bunukangoma katika Kata Kahororo, katika Manispaaya Bukoba, Wilson Masaba, akiangalia nyumba yake iliyoezuliwa na upepo mkali juzi. Picha na Lilian Rugakingila 

Mkazi wa Mtaa wa Bunukangoma katika Kata Kahororo, katika Manispaaya Bukoba, Wilson Masaba, akiangalia nyumba yake iliyoezuliwa na upepo mkali juzi. Picha na Lilian Rugakingila

MANDELA APATA FARAJA HOSPITALINI


Raia wa Afrika Kusini akiwa na bango la kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Mstaafu wa nchi hiyo, mjini Polokwane nchini humo. Picha na Mtandao 

UMAARUFU HAUJI KIZEMBE


Mwigizaji anayechipukia, Mariam Ismail amesema umaarufu wa msanii hauji kwa kuandikwa vibaya na vyombo vya habari, bali ni kutokana na sifa alizonazo katika kazi yake ya sanaa.

 

“Umaarufu wa msanii si lazima ajengwe kwa kuandikwa kashfa katika vyombo vya habari bali ni kuitendea haki filamu anayochaguliwa.”

 

Mariam anaamini anafanya hivyo katika filamu anazocheza kila anapochaguliwa jambo ambalo hivi sasa kila mtayarishaji anahitaji kufanya naye kazi kwa sababu anajua.

 

Alisema wasanii wengi hasa wa filamu wamekuwa na tabia ya kutengeneza kashfa na wakati mwingine kuvaa nusu uchi ili tu watokeze kwenye vyombo vya habari jambo ambalo linawashushia heshima katika jamii.

 

“Wasanii tumekuwa na tabia ya kutokujijali, watu wanavaa nusu uchi na malengo yao hasa ni kutokea kwenye vyombo vya habari,” alisema Mariam. Na Herieth Makwetta

 

Jumatatu, 15 Julai 2013

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YA ANDAA MFUKO WA KULINDA MLIMA KILIMANJARO DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.


WIZARA ya Maliasili na Utalii, imeanza mchakato wa kuandaa mfuko wa kulinda Mlima Kilimanjaro dhidi ya majanga ya moto pamoja na uandaaji wa rasimu ya mfumo maalumu unaoshirikisha kada mbalimbali kwenye ulinzi wa hifadhi za taifa.


Wizara imefikia hatua hiyo kutokana na kuwapo kwa matukio ya moto ya mara kwa mara katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, yanayodaiwa kusababishwa na shughuli za kurina asali ndani ya hifadhi hiyo.

 

 Akizungumza na uongozi wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro na vikosi vya askari mgambo na askari polisi wa Chuo cha Polisi Moshi walioshiriki zoezi la kuzima moto katika mlima huo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema mfumo huo utakuwa shirikishi.

 

“Mfumo huu utakuwa ni shirikishi na utawahusisha wananchi katika vijiji vinavyozunguka hifadhi na pia utazihusisha halmashauri za wilaya. Sasa hili liko kwenye mchakato na sasa tunaandaa rasimu ya uendeshaji wa mfumo huo,” alisema Nyalandu.

 

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC), ambazo zinaingizwa kwenye mfumo unaoanzishwa wa kutambua moto kwa njia ya satellite, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwezesha wakuu wa hifadhi kuweza kubaini matukio hayo kabla hayajaleta maafa makubwa zaidi.

 

Katika hatua nyingine, Nyalandu alitoa agizo la kuzuia utoaji wa vibali vya kuvuna kuni na urinaji asali ndani ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na badala yake vitatolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

 

Katika agizo hilo, Nyalandu alisema uamuzi huo unatokana na matokeo ya utafiti wa majanga ya moto ndani ya hifadhi hiyo kuonyesha kuwa chanzo kikuu ni urinaji wa asali au uvunaji wa kuni unaofanywa na baadhi ya wananchi waishio vijiji jirani.

 

Nyalandu alisema amri hiyo ya serikali inapaswa kuheshimiwa na kila mmoja, na akaonya hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale watakaobainika kuikiuka.

 

Awali Mhifadhi Mkuu wa KINAPA, Erastus Lufungulo, alisema moto uliobainika Jumapili iliyopita, umeteketeza eneo la hekari 40 na kwamba juhudi za kuudhibiti zilizaa matunda baada ya kupata msaada wa askari mgambo kutoka wilaya zote mkoani hapa

 

Na Dixon Busagaga

MBOEWE ADAI POLISI WALIVAMIA USIKU MAKAZI YAKE D’SALAAM



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe 

Polisi kadhaa wanadaiwa kuvamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kwa lengo la kumkamata. 

 

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mbowe mwenyewe zinaeleza kuwa askari hao waliokuwa na silaha walivamia nyumba hiyo iliyopo eneo la Mikocheni, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana wakiwa na silaha.

 

Mbowe alisema hata hivyo walikwama kumkamata, kwa sababu alikuwa nje ya Dar es Salaam kwa shughuli za chama.

 

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alikataa kuzungumzia zaidi suala hilo akieleza kuwa anayeweza kulizungumzia zaidi ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillius Wambura alipoulizwa alisema kuwa hana taarifa za polisi kumtafuta Mbowe.

 

“Sina taarifa polisi wangu kumtafuta Mbowe,” alisema Wambura.

 

Lakini Ofisa Habari wa Chadema Tumaini Makene aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa askari hao walifika nyumbani kwa Mbowe saa 7:16 usiku, wakidai kuwa na hati ya kumkamata Mbowe kutokana na makosa ambayo hata hivyo hawakuyabainisha.

 

“Ni kweli askari walifika nyumbani kwa Mwenyekiti wakidai walikuwa wakihitaji kumkamata. Kinachotushangaza ni kwamba mtu ambaye anafahamika na wanajua ni mbunge na kiongozi wa chama, lakini wanakwenda kumkamata kama jambazi, usiku wa manane,” alisema Makene.

 

Alisema kuwa polisi hao walifika nyumbani kwa Mbowe na kukutana na walinzi katika nyumba hiyo, waliowaeleza kuwa mwenyekiti huyo wa Chadema alikuwa safarini.

 

Makene hakuwataja majina walinzi waliokutwa , lakini nalisisitiza kwamba polisi hao waliacha namba za simu kwa walinzi hao, wakitoa maelezo kuwa pindi Mbowe atakaporejea wamwarifu na kuwapigia polisi kwa kuwa alikuwa akihitajika kituoni.

 

Ofisa huyo alieleza kuwa wakati wa tukio hilo Mbowe hakuwapo nyumbani na alikuwa safarini mkoani Kilimanjaro, kuhudhuria vikao vya Halmashauri ya Hai.

 

Makene alisema wanashangazwa na vitendo vya Polisi kusaka viongozi wao usiku wa manane kama majambazi sugu, wakati wakifahamika ni wabunge.

MGOMBEA UWT TAIFA, MAGIGE AONYESHA KADI YA CHADEMA


Aliyekuwa mgombea UWT Taifa, Maryrose Magige akionyesha kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi Manzese Dar es Salaam jana. Picha na Salim Shao 

CHADEMA WANASA WARAKA WA SIRI WA CCM

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kunasa waraka wa siri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaokwenda kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Warioba, ukimshinikiza kukubali mapendekezo yao.


Waraka huo wa CCM uliosainiwa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Jitu Vrajilal Soni una lengo la kupinga mapendekezo mbalimbali yaliyomo katika Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyozinduliwa Juni 3 mwaka huu.


Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Mashariki na Pwani, Mabere Marando akihutubia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja cha Shule ya Msingi Ukombozi, Manzese jijini jana alidai waraka huo una lengo la kuvuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya yenye manufaa kwa Watanzania wote.

 

Marando akisoma baadhi ya mapendekezo ya CCM yaliyomo katika waraka huo kwenda kwa Jaji Warioba kumtaka kuviondoa vipengele vilivyomo ndani ya Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya vinavyohusu Tunu ya Taifa, kuwa bila kufanya hivyo hakutakuwa na tija ya uwajibikaji.


Alizitaja tunu hizo za taifa kuwa ni kuwa utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa ambazo Chadema wanaziunga mkono zipite na kuwa sheria.


“Sisi Chadema tunaona zinafaa kutokana na umuhimu wake lakini CCM wamemwambia Warioba aondoe neno uwazi wakiwa na maana ya kuwa wanataka mambo yao yasiwekwe wazi,” alisema Marando.


Marando ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema, Jaji Warioba amependekeza utajiri wa taifa uendelezwe na kuzuia mtu kumnyonya mwenzake jambo ambalo CCM wamelipinga.


“CCM katika waraka huo ibara ya 11.2 na 11.3 wamemwambia Warioba viondolewe, sasa viongozi wa CCM na Chadema ni kina nani wanawapenda wananchi wake,” aliwauliza wananchi waliojitokeza katika mkutano huo na kujibiwa na kelele kuwa ni Chadema.


Marando alisema katika kipengele cha maadili ya taifa na jamii kinachosema viongozi wanatakiwa kuzingatia uongozi, utoaji wa huduma, kufanya usawa na kupiga vita rushwa mapendekezo ambayo yakipita kuwa sheria yatasaidia kupunguza tatizo la rushwa la utoaji wa huduma uliotukuta.

 

“CCM ambao hawaonyeshi dhamira ya kumkomboa mwananchi wake, wamemwambia Warioba kuyaondoa maadili hayo kwani hayafai, sasa kupiga watu, kula rushwa kweli liondolewe? Hawa CCM kweli hawataki tupate katiba ya kuwakomboa wananchi,” alisema Marando na kuongeza:

 

“Kama hiyo haitoshi wamesema kitendo cha wananchi kumwajibisha mbunge wao kama hatakuwa anatimiza majukumu yake nao wamesema mapendekezo hayo hayafai. Kweli CCM hawataki tupate Katiba Mpya.”

 

SHEIKH WA WILAYA ARUSHIWA TINDIKALI



Wakati vumbi la matukio ya kigaidi ya milipuko ya bomu kanisani na kwenye mkutano wa kampeni za Chadema halijatulia, tukio lingine linalohusishwa na ugaidi limetokea wilayani Arumeru kwa Sheikh wa wilaya hiyo, Said Juma Makamba aliyejeruhiwa kwa kumwagiwa usoni kimiminika kinachoaminika kuwa tindikali.

 

Sheikh Makamba anayekaimu nafasi hiyo alikutwa na hayo kati ya Saa 4:00 hadi 5:00 usiku wa kuamkia juzi akitoka kusali Tarawei na alilazwa wodi namba nne katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa matibabu.

 

Jicho la kushoto la Sheikh huyo limeathirika, huku akiwa amebabuka na kuvimba usoni, kifuani, mkono wa kushoto na mgongoni.

 

Akizungumza kwa taabu kitandani kwake alikolazwa, Sheikh Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei wilayani Arumeru alisema alimwagiwa tindikali muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake akitoka kuswali.

 

“Nilipotoka Msikitini, nilisindikizwa hadi nyumbani na vijana wawili nilioongozana nao kutoka msikitini ambao walihakikisha nimeingia ndani salama. Lakini kabla ya kulala nilitoka nje kwa ajili ya kujisaidia kwenye choo cha nje ndipo nilimwona mtu amesimama pembeni ya nyumba nikiwa najitahidi kumwangalia ili nimtambue, ghafla alinimwagia kitu cha majimaji usoni,” alisema Sheikh Makamba.

 

Ingawa hataki kuingia kwa undani kuhusu anaowatuhumu na sababu za kumwagiwa tindikali, Sheikh Makamba alisema anadhani jambo hilo linatoakana na ugomvi wa madaraka msikitini hapo.

 

Katibu wa Bakwata Wilaya ya Arumeru, Sheikh Yahaya Husein Mwangela aliwaomba polisi kuchunguza tukio hilo ili kuondoa hofu miongoni mwa viongozi wa Bakwata.

 

Hili ni tukio la pili kwa viongozi wa Bakwata Arusha kumwagiwa tindikali baada ya Oktoba mwaka jana, Katibu wa Baraza hilo Mkoa wa Arusha, Abdukarim Njonjo kulipuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu. Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa hadi juzi kulikuwa hakuna mtu aliyekamatwa.

 

ri imeanza upelelezi na uchunguzi wa kina wa tukio hilo kubaini wahusika.

 

Hadi jana jioni, hakuna mtu aliyekuwa akishikiliwa polisi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.

 

USHOGA, UCHANGUDOA MAANGAMIZO MENGINE BUGURUNI NA VINGUNGUTI



Asilimia 65 ya vijana kata za Buguruni na Vingunguti wapo hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na kujihusisha na biashara ya ushoga na uchangudoa. 

 

Katika utafiti uliofanywa na Shirika la Ushauri kwa Familia (CAFLO) mwishoni mwa mwaka jana, uneonyesha idadi kubwa ya vijana hao ni wenye umri kuanzia miaka 12 na kuendelea.

 

Akizungumza kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana na watu wanaoishi na VVU kutoka maeneo hayo juzi, Mwenyekiti wa shirika hilo, Mariam Mlugu, alisema idadi kubwa ya vijana hao ni wale waliochukuliwa kutoka mikoani kufanya kazi za ndani.

 

Mlugu alisema baada ya kufika Dar es Salaam, vijana hao wamejikuta wakiingia kwenye biashara hizo kutokana na unyanyasaji na ujira mdogo.

 

Alisema baada ya utafiti huo waliwasiliana na Kamati ya Ukimwi Manispaa ya Ilala ambayo ilikubali kuliwezesha shirika hilo kutoa mafunzo kwa vijana na wanaoishi na VVU, ili wabuni na kutafuta fursa mbalimbali kujiletea maendeleo.

 

Pia, Mlugu alisema baadhi ya  familia na jamii zimekuwa zikikosa fursa kufanya shughuli halali na kuamua kujiingiza kwenye kazi hatarishi, kama  biashara ya ngono na mapenzi ya jinsia moja kwa lengo la kujipatia kipato.

 

Awali, Mkurugenzi wa utawala wa shirika hilo, Dennis Mikongoti, alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo watu wanaoishi na VVU na Ukimwi na ambao wapo hatarini kupata magonjwa hayo,  ili wapambane na umaskini wa kipato ambao ndiyo unachangia kwa kasi maambukizi hayo. Naye

 

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Ilala, Malcela Msawanga, aliwaasa washiriki hao kutumia mafunzo hayo kuwaelimisha wenzao ambao hawakupata fursa hiyo.

 

 

MADEREVA WA BODABODA WAFANYA NGONO NA WANAFUNZI, WALIMU NA WAKE ZA WATU



Imebainika kuwa baadhi ya madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wanatumia usafiri huo kuwarubuni na kuwashawishi wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari na kufanya nao ngono.

 

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili jijini Dar es Salaam katika Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondononi, umebaini kuwa wanafunzi wengi wamejiingiza katika vitendo vya ngono baada ya kunaswa na ulaghai wa madreva bodaboda wengi wakiwa vijana wadogo.

 

Madereva hao wamekuwa wakifanya ngono na wanafunzi, baada ya kuahidi kuwasafirisha bure kwenda na kurudi kutoka shuleni, hasa kwa maeneo ambayo hakuna usafiri wa daladala au eneo lililo mbali na kituo cha basi wakati wa kutoka au kwenda shuleni.

 

Gazeti hili limebaini kwamba, baadhi ya walimu pia wamejiingiza katika mchezo huo mchafu na kufanya ngono na vijana wadogo wanaoendesha bodaboda.

 

Madereva hao wanaoonekana katika vituo vya daladala, huwafuata wanafunzi hao wanaosumbuliwa na shida ya usafiri wakikataliwa kupanda daladala makondakta wa daladala hasa wakati wa asubuhi na jioni.

 

“Njoo asubuhi utaona wanafunzi wanavyohangaika kupata usafiri, mtu amefika kituoni toka saa kumi na mbili hadi saa mbili bado yupo hapa kila basi linalokuja anaambiwa wanafunzi wametosha. Katika mazingira haya kwanini asirubuniwe na mtu wa bodaboda?” alihoji mmoja wa wazazi alijitambulisha kwa jina la Mwambene na kuongeza:

 

 “Kuna baadhi ya madereva ninawafahamu wana uhusiano na wanafunzi wawili hadi watatu, tena hawachagui mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari, lazima wazazi wawafuatilie watoto wao vinginevyo wanafunzi hawatamaliza masomo.”


Baadhi ya madereva bodaboda walisimulia wanavyowashawishi na kuwanasa wanafunzi, wakikiri kulitumia tatizo la usafiri wa kwenda na kurudi kutoka shuleni kuwapata kirahisi wanafunzi.

 

Akionekana kuvifurahia vitendo hivyo, mmoja wa madereva wa bodaboda katika kituo cha daladala cha Temeke mwisho, (jina tunalo) alisema baadhi ya wanafunzi wanaona ufahari kupelekwa shuleni kwa pikipiki jambo linalowafanya wawe tayari kukubali kufanya ngono.


“Wapo wanafunzi wanaopenda kuonekana wanatoka katika familia bora, ...hao ndiyo rahisi sana kuwapata, ukimpeleka shuleni mara ya kwanza, mara ya pili basi umemaliza mchezo,” alisema dereva huyo akijinasibu.


Alisema baadhi ya wanafunzi hutoka nyumbani kwao wakiaga wanakwenda shuleni lakini badala yake hukutana na madereva wa bodaboda ambao huwapeleka mafichoni na kufanya nao ngono


TFDA ilitoa taarifa kwamba mafta ya ubuyu  hayafai kwa matumizi ya binadamu kwa sababu yana kiwango kikubwa cha tindikali ya mafuta aina ya Cyclopropenoic fatty acids.Pia ilisema ili yaweze kukidhi vigezo vya ubora na usalama ni lazima yafanyiwe usafishaji wakati wa usindikaji na kwa sasa nchini hakuna aina ya usindikaji huo.

SASA NI KATI YA CHAMA CHA TIBA ASILI (ATME) NA TDFA.


Mafuta ya ubuyu

 

Mratibu wa Chama cha Watabibu wa Dawa za Asili Tanzania (ATME), Boniventure Mwalongo amesema taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TDFA) kuhusu matumizi ya mafuta ya ubuyu zinaweza kuleta madhara kwa jamii kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiyatumia.

Akitolea mfano watumiaji wakubwa  wa mafuta hayo, Mwalongo alisema, wenye magonjwa kama ya moyo na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wamekuwa wakiyatumia mafuta hayo kwa muda mrefu na kudai yamewasaidia.

 

Mwalongo ameyasema hayo jana baada ya hivi karibuni kuibuka utata kuhusu ubora na usalama wa mafuta hayo na kudai kuwa wao kama ATME walianza kuyatumia kama dawa kwa wateja wao siku nyingi na hawajawahi kupata malalamiko yoyote na kuwahakikishia watumiaji kuwa hayana madhara.

 

 “Yametumika kwa zaidi ya miaka 20 na sisi tunazo kumbukumbu za wagonjwa tuliowapa mafuta hayo kama dawa na hatujawahi kupata ripoti yoyote ya madhara kwa wale waliotumia,” alisema Mwalongo.   TFDA ilitoa taarifa kwamba mafuta hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu kwa sababu yana kiwango kikubwa cha tindikali ya mafuta aina ya cyclopropenoic fatty acids.

 

Katika taarifa ya TFDA iliyotolewa juma lililopita ilisema athari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi ya mafuta hayo ni pamoja na kuathiri vimeng’enyo vinavyosaidia katika uchakataji wa tindikali za mafuta mwilini. 

 

Pia ilisema ili yaweze kukidhi vigezo vya ubora na usalama ni lazima yafanyiwe usafishaji wakati wa usindikaji na kwamba kwa sasa nchini hakuna aina ya usindikaji unaofanyika wenye uwezo wa kuondoa tindikali hiyo ya cyclopropenoic fatty acids katika mafuta ya mbegu za ubuyu.

 

Hata hivyo Mwalongo alikemea usambazaji holela wa mafuta hayo hasa baada ya kubainika kuwa yanatibu maradhi mbalimbali ambapo baadhi ya wajasiriamali wamekuwa wakiyasambaza wakati siyo wataalamu wa tiba asili.

 

Mratibu huyo alizishauri mamlaka zinazohusika na suala zima la afya ya binadamu nchini kutoa majibu yatakayosaidia kuondoa mgawanyiko uliopo sasa kutokana na mafuta hayo badala ya kutoa taarifa za kutisha.


Hata hivyo alipoulizwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Paul Mhame, alisema hawana taarifa zozote kama kuna tafiti zimefanyika kuhusiana na matumizi ya mafuta hayo.

JWTZ KUCHUNGUZA MAUAJI YA WANAJESHI

Wakati Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban K-Moon, wamelaani mauaji ya wanajeshi wa Tanzania Jimbo la Darfur, Sudan,  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeunda timu ya kuchunguza tukio hilo

 

Wapiganaji saba kati ya 36 wa Tanzania waliokuwa kwenye Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa, (Unamid), waliuawa  Jumamosi na wengine 19 kujeruhiwa.

Mashambulizi hayo yalitekelezwa karibu na kambi ya Manawashi eneo la Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala.

 

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema Dar es Salaam jana kuwa timu ya wataalamu itakwenda Darfur kuchunguza tukio hilo.

 

Tukio hilo limekuwa la kushtua, kwani miaka mitano ya majeshi ya kulinda amani kuwa huko haijawahi kutokea mauaji makubwa kiasi kile.

 Kanali Mgawe alisema wanawasiliana na UN kufanya taratibu za kurudisha nyumbani miili ya wapiganaji hao.

 

Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Unamid, Christopher Cycmanick,   ilisema wanajeshi hao waliuawa walipokuwa kwenye doria ya kawaida.

 

Cycmanick alisema walinzi hao wa amani walishambuliwa kwa bunduki na silaha nzito za kivita umbali wa kilomita 25 kutoka katika kambi yao.

 

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais Kikwete ameeleza kushtushwa na tukio la kushambuliwa na kuuawa wapiganaji wa JWTZ Mji wa Darfur, Sudan.

 

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu, ilisema Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, familia na wapiganaji wote.

CHADEMA YA ITESA CCM UCHAGUZI WA UDIWANI ARUSHA

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)wakiimarisha ulinzi kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kaloleni wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo uliofanyika jana.Picha na Filbert Rweyemamu.

Jumamosi, 13 Julai 2013

Wafuasi wa Morsi waandamana Cairo

Watu watano wameuawa kwenye shambulio la bomu la kujilipua, lililolenga wanajeshi wa kutunza amani wa Muungano wa Afrika mjini Mogadishu, Somalia. 
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, ameiambia BBC kuwa ameona miili ya raia watano, ambao walikufa baada ya bomu hilo lililokuwa ndani ya gari kulipuka.
Muungano wa Afrika umethibitisha kuwa wanajeshi wake wawili walijeruhiwa kwenye shambulio hilo.
Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo la Bomu, lakini kundi la Al shabaab lililo na uhusiano na kundi la kigaidi ya Al-Qaeda limewahi kufanya mashambulio kama hayo mjini Mogadishu.
Kundi hilo la Al-Shabab, linataka kuundwa kwa taifa la Kiislamu la Somalia, licha ya kuwa wapiganaji wake wametimuliwa kutoka mji mkuu wa nchi hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Al Shabaab bado linadhibiti maeneo kadhaa ya Somalia.
Zaidi ya wanajeshi elfu kumi na nane wa Muungano wa Afrika wako nchini Somalia, kuisaidia serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na rais Hassan Sheikh Mohamud, ambaye alichaguliwa na wabunge September mwaka uliopita(bbc)