Alhamisi, 4 Julai 2013

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA SOKA MKOANI MBEYA (MREFA) HAROUB SULEIMANI AKANUSHA MADAI


Timu ya soka ya mkoa wa Mara Polisi jamii bunda ambayo inashiriki michuano ya mabingwa wa mikoa nchini   imewasirisha rufaa kwenye shirikisho la  soka nchini TFF Julai 3, mwaka huu.

 

Polisi bunda kupitia chama cha soka mkoani Mara walituma malalamiko yanayo ishutumu timu ya kimondo fc ya mkoani Mbeya kwa kupanga mchezo wao wa marudiano kufanyika siku ya jumamosi badala ya jumapili kama shirikisho la soka nchini lililivyo amuru kuwa machezo yote ifanyike juni 30 siku ya jumapili.

 

Aidha akiongea Baragumu katibu mkuu wa  chama cha soka mkoani Mbeya (MREFA) Haroub Suleiman amekanusha madai hayo kwa kusema kuwa shirikisho la soka nchini limezipa uhuru timu wenyeji katika michuano hiyo kuamua siku hususa ya mchezo kati ya siku mbili za miisho juma ili kucheza michzo yake.

 


Pia Haroub alisema kuwa aliwasiliana na viongozi wa timu ya Polisi bunda na kuwajulisha siku ya mchezo wao dhidi ya kimondo kuwa ni jumamosi na ndio sababu walicheza siku hiyo bila kipingamizi, katika  mchezo huo kimondo iliibugiza timu hiyo ya Polisi bunda kwa magoli (3-1)katika uwanja wa kumbu kumbu ya sokoine jijini hapa.

SEKRETARIETI YA MKOA WA MBEYA YAPENDEKEZA JINA LA MKOA MPYA

               

Sekretarieti ya mkoa wa Mbeya imependekeza mkoa mpya utakaoanzishwa uitwe mkoa wa Songwe na makao makuu yake yakiwa Mkwajuni wilayani Chunya.

 

Mapendekezo hayo yametolewa julai 4 mwaka huu katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa iliyohusisha wajumbe kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya iliyofanyika katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya.

 

Akizungumza kwaniaba ya wajumbe mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbasi Kandoro amesema kuwa wamependekeza mkoa mpya uitwe SONGWE kwa kuzingatia vigezo vilivyo tolewa na ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa

 

Aidha Kandoro amesema kuwa mkoa mpya wa Songwe utaundwa na wilaya za Ileje,Chunya,Mbozi na Momba na makao makuu yake yakiwa ni Mkwajuni wilayani Chunya wakati mkoa Mbeya utabaki na wilaya za Mbeya,Rungwe,Mbalali na Kyela.

 

 Hata hivyo wasema kuwa lengo la kuugawa mkoa ni kutokana na mkoa wa Mbeya kuwa na eneo kubwa hivyo linastahili kutoa mikoa miwili ili kuboresha huduma kwa wananchi na kuongeza kasi ya ukuaji wa kiuchumi.

CCM YA PATA PIGO


 Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimeendelea kupata pigo kubwa baada ya kifo cha diwani wa kata ya Nduli, katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Idd Chonanga.

 

Chonanga alifariki dunia july 3 mwaka huu na kufikisha idadi ya madiwani 8 wa CCM kupoteza maisha kwa kipindi hiki cha miaka mitatu pekee

 

Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa, Aman Mwamwindi alithibitisha kutokea kwa kifo cha diwani Chonanga na kusema kuwa kifo hicho kilitokea majira ya saa 8 mchana siku ya july 3 katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo diwani huyo alilazwa.

 

Mwamwindi alisema kuwa Chonanga alifikishwa Hospitalini hapo majira ya saa 12 asubuhi kutokana na tatizo la ugonjwa wa BP ya kushuka, na madaktari walijitahidi kuhangaikia kuokoa maisha yake, lakini ilipofika majira ya saa 8 mchana diwani huyo alifariki dunia.

 

Hata hivyo Mwamwindi alisema kuwa kifo cha diwani Chonanga ni pigo kubwa ndani ya halmashauri ya manispaa ya Iringa kutokana na utendaji kazi wa diwani huyo katika Halmashauri hiyo kupitia kata yake ya Nduli.

  

AMEPOTEZA MAISHA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI


Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika alipoteza maisha baada ya kugongwa na trini eneo la darajani Uyole jijini Mbeya julai 02, 2013 majira ya saa tano asubuhi.


Wakizungumza na Baragumu mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa marehemu amefikwa na mauti majira ya saa tano asubuhi alipokuwa amekaa juu ya reli.


Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mashuhuda Thimosi seme alisema marehemu alikuwa amekaa relini ndipo treni ikampitia na kusababisha kifo chake papo hapo.


Naye shuhuda mwingine jina lake litajwe dereva pikipiki alisema kuwa hakujua kinachoendelea wakati Treni inapita gafla mtu mmoja alitoka juu ya reli na kutoa taarifa ya mtu aliyegongwa na treni ndio kwenda kutazama.


Mpaka majira ya saa saba hakuna ndugu aliyefika kuutambua mwili wa marehemu na hata hivyo kwa wakati huo alifika askali wa usalama barabarani na baada ya kuhojiwa alisema hawezi kuzungumzia chochote kuhusu ajali hiyo.


Kulingana na tukio hilo kisheria marehemu amegonga Treni

Jumanne, 2 Julai 2013

KIWANDA CHA KUSAFISHIA MADINI YA DHAHABU KINACHO KILICHOPO GOMBE KUSINI MKOANI MBEYA KIKIMILIKIWA NA STEWART MWITA KIMEIBUA JIPYA

wananchi wa Gombe kusini mkoani Mbeya wamelalamikia uwepo wa kiwanda cha kusafishia madini ya dhahabu kinachomilikiwa na Stewart Mwita wakidai kuwa kimekuwa kikitiririsha moshi na kusababisha harufu kali ambayo walisema ni kero na hatari kwa afya za wananchi wa eneo hilo.

 

Wakizungumza na Baragumu wananchi hao walisema kuwa, kiwanda hicho kinatoa sumu ambayo ina madhara makubwa kwa watu wa eneo hilo ikiwemo kukohoa mara kwa mara.

 

Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Godfrei Kapunga alisema kuwa taarifa walizitoa katika ofisi ya Mkoa na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya kiwanda hicho.

 

Akizungumzia suala hilo Afisa wa madini Mkoa wa Mbeya, alisema kuwa madhara yanayo sababishwa na utiririshwaji wa maji taka kutoka katika kiwanda hicho yanaweza kusababisha madhara hasi kwa wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho ambacho wanaathirika na maji hayo taka yenye kemikali kama vile mekyuri ambazo zinaweza kuwa hatari kwa binadamu.

 

Afisa madini alisema kiwanda hicho kinapaswa kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira au la uongozi wa Mkoa utalazimika kukiondoa katika eneo hilo iwapo itabainika kimejengwa jirani na makazi ya watu.

 

Wakitoa maoni yao wananchi wa mtaa wa Gombe kusini walisema kuwa wanaomba kiwanda hicho kiondolewe maramoja, pia wanaomba kupimwa afya zao na kwamba iwapo watabainika kupata madhara kutokana na taka za kiwanda hicho basi watadai fidia.

MCHUNGAJI AFUNGWA JELA MIAKA 30 BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KUMBAKA MWANAFUNZI

Mahakama ya hakimu mfadhiwa wilaya ya Mbeya imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela mchungaji wa kanisa la Evangelical Assembliss of God (EAGT) Daniel mwasumbi (57) mkazi wa jijini Mbeya baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi (19)

Hukumu hiyo imwtolewa na hakimu wa kesi hiyo Gilbert Ndeulo, baada ya kusikilizwa kwa ushahidi wa pande zote mblili za kesi hiyo mbele ya aliyekuwa mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Achiles Mlisa.

 

Kabla ya kutoa hukumu ya kesi hiyo hakimu Ndeoluo alisima kuwa mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita (6) na vielelezo kadhaa vya upande wa mashtaka alianza mahusiano na binti huyo akiwa na umri wa miaka 15 baada ya bimti huyo kumaliza elimu yake ya msingi.

 

Hakimu Gilbert Ndeuluo alisema kuwa aliyekiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la kumbaka mhanga kinyume cha sheria No. 130 kifungu kidogo cha sheria No.5 sura ya 16.

 

Hakimu Ndeuluo alisema kuwa mchungaji Mwasumbi alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo kwa zaidi ya miaka minne hali iliyopelekea mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari Itende iliyopo jijini mbeya kupata ujauzito na kujifungua mtoto wa kwa mnamo aprili 2010 na kuacha masomo yake.

 

OBAMA AFURAHIA KUITEMBELEA TANZANIA

Rais Barack Obama akisalimiana na watanzania mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam Julai Mosi.PICHA THE WASHINGTON POST