Jumanne, 26 Mei 2015

MATOKEO YA BALEHE NI HAYA NA ELIMU YA JINSIA SOMA HAPA


Kuna mabadiliko ya kimwili ambayo hutokea wakati wa kubalehe. Mabadiliko haya ni pamoja na ukuaji na utanukaji wa viungo vya uzazi au jinsia. Wanaume na wanawake wana viungo vya uzazi ambavyo vinaweza kuonekana nje ya miili yao. Wanawake pia wana viungo vya sehemu za siri ndani ya mwili. Viungo hivyo vyote vilivyopo ndani ya mwili huitwa viungo vya ndani ya uzazi na vile vilivyopo nje huitwa ni sehemu za siri.
Viungo vya uzazi vya kike:
Wanawake  wana  njia tatu ndogo katikati ya miguu yao. Mbele kuna njia  iitwayo urethral  ambayo huitumia kwa ajili ya haja ndogo. Njia ya haja kubwa (anus) ambayo ipo nyuma ambayo huitumia kwa ajili ya kwenda haja kubwa na katikati  kuna mlango ambao unaingia  katika viungo vya ndani vya sehemu ya uzazi (Vagina).Wakati mwanamke anapokuwa katika siku zake  damu hutoka nje kwa njia  hiyo ya katikati. 
Ndani ya uke  kuna  ngozi nyembamba iitwayo hymen. Hymen sehemu ya  kazi yake ni kuzuia  uke, lakini bado  kunakuwepo na nafasi ya kutosha ili kuweza damu  kupita.
Kiungo kingine muhimu ni kisimi au kinembe (clitoris). Hiki kina ukubwa wa kila aina na kipo mbele ya kiungo cha nje cha uke wa  mwanamke.  Kiungo hiki ni chombo nyeti sana sawa na viungo vingine nyeti kwa mwanamme na husaidia mwanamke kujisikia furaha wakati wakiburudishana na mumewe. Midomo ya nje ya viungo vya mwanamke (labia)  pamoja na kisimi na uwazi wa uke inajulikana kama uke.
Viungo vya uzazi vya kiume:
Kwa upande wa mwanamume, viungo vya nje vya uzazi  ni uume na vifuko viwili (korodani) ambavyo  vinaweza kuitwa kiwanda  cha kuzalisha mbegu za kiume ingawa  kwa lugha ya kitaalamu vinaitwa “pair of testes” (ama wakati mwingine uitwa  testicles) Vifuko hivi viwili vipo chini ya kibofu na vimefungwa pamoja kama mfano wa pochi ambao kwa lugha pia ya kitaalamu unajulukana kama ‘scrotum ama scrotal sac’.
Uume ni  chombo ambacho kinaruhusu kupenya ndani ya uke. Uume unaundwa na misuli myembamba sana (tissue spongy) .
Wakati misuli hiyo inapokuwa imejaa sambamba na damu uume unakuwa imara. Wakati kunapokuwa hakuna tendo la ndoa uume upoteza uimara wake  na  damu ya ziada huenda kutumika kwenye viungo vingine vya mwili  na uume unakuwa umesinyaa.

BAADA YA WANAUME KUSHINDWA KUWARIDHISHA WAPENZI WAO KUNANJIA YA MBADALA INAYOPENDEKEZWA ISOME HAPA CHINI

150425160726_miraa_640x360_bbc_nocredit



Baada ya wanaume kushindwa kuwaridhisha wapezi wao kunanjia mbadala iliyopendekezwa
Wanaume katika eneo la Meru mashariki mwa Kenya ambao wanasadikiwa kuwa hawana uwezo wa kuwatosheleza wake zao kupitia tendo la ngono sasa wametakiwa kutokuwa na wasiwasi.
Mwakilishi wa wanawake katika eneo hilo Florence kajuju ameanza mpango wa kuwahamasisha wanaume kutumia miraa badala ya ya pombe haramu .
Akizungumza na gazeti la The Nairobian nchini Kenya,kiongozi huyo amesema kuwa pombe haramu hushusha nguvu za kiume na kuwafanya wanaume kushindwa kuwatosheleza wake zao.
”Ni pombe kama hizi ambazo huathiri nguvu za kiume na kusababisha utasa miongoni mwa wanaume”,alisema.
Kajuju ambaye anasema anapenda miraa aliudhika alipogundua kwamba eneo la Meru ni miongoni mwa maeneo ambayo wanaume hawana uwezo wa kutafuta watoto.
”Vijana wetu wameathirika vibaya na pombe haramu na lazima tuwaokoe”.
Alisema kuwa wale waliopiga marufuku uuzaji wa miraa katika mataifa yao wanafaa kugundua umuhimu wa zao hilo miongoni mwa jamii.

Jumatatu, 25 Mei 2015

KWA NINI WATU WEMA KUFANYA MAMBO MABAYA

Hayden Christensen as Anakin Skywalker in Star Wars: Episode II -- Attack of the Clones, before giving into temptation and joining the Dark Side as Darth Vader.

Wengi wetu hatupendi kufanya mambo mabaya mfano kudaganya, kuiba, kuenda kinyume na utaratibu uliowekwa kwa kuhofia kuonekana vibaya au aibu itakayo tokea baadae hivyo huji taidi asikosee, lakini imeonekana kwamba majaribu haya wanayo kutana nayo yakizidi au kuonekana kuwa kama jambo dogo mbele ya jambo kubwa hivyo hulazimika kudanganya au kufanya jambo ilo baya ili tu afanikishe jambo lake mfano anapotaka kufanya jambo kubwa asilokuwa na uwezo nalo, muda pia huchangia sana mtu mwema kutenda jambo baya mfano mtu anataka kukitu kwa wakati na pesa hana inabidi adanganye tu ili apate, tena akiwa na mfululizo wa mambo magumu huchangia sana afanye jambo kinyume na sifa aliye nayo. 

Pia ni kushindwa kwao kukabiliana na kutambua kuna majaribu, Mbali na kukiri majaribu, utafiti unaonyesha kuwa watu kuwa na kuona kama moja wapate sababu ya mapambano na tena na tena, na kwamba inaweza uwezekano wa kuhatarisha sifa na uadilifu wao. Katika mtihani wa kwanza. 

Utafiti mwingine unaonyesha kuwa kuwakumbusha kuhusu majaribu yanaweza kuimarisha kujizuia katika maeneo mengine pia kupingwa pingwa katika maamuzi ambayo huyu mtu mwema anakua anayatoa hivyo atafanya ajidharau naamue kufanya jambo lolote baya kutafuta suruhishi tu. Kuandamwa na kesi za mara kwa mara pia huwa changizo kubwa sana.

 

Jumanne, 26 Agosti 2014

WAZAZI WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA ELIMU



Wazazi na walezi wametakiwa kuwekeza katika elimu ya watoto kwa kuwa kufanya hivyo ndiyo bima pekee bora kwa maisha yao ya baadaye na Taifa kwa jumla. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Naweza Kufikiri, Naweza Kuzungumza.

 Mashindano hayo yanashirikisha wanafunzi zaidi ya 100 kutoka shule 37 za sekondari wilayani Mufindi na lengo la kuanzishwa ni kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri.Mhagama alisema wakati umefika kwa Watanzania kuwekeza katika elimu ili kulikomboa Taifa kutoka katika umaskini, ujinga na maradhi.

 

Jumamosi, 23 Agosti 2014

BEN POL: SIHITAJI KWENDA NJE YA NCHI


 

Ben Paul 


Wakati wasanii wengine wakifanya juhudi kuhakikisha wanasafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutengeneza video za nyimbo zao,, mwimbaji mwenye sauti ya kuvutia, Bernard Paul maarufu ‘Ben Pol’ amesema kuwa hana mpango wa kutengeneza video nje ya Tanzania.

 

Ben Pol amesema licha ya video zake nyingi kuwa amezifanyia hapa nchini, lakini zimefanikiwa kuonyeshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni Afrika Kusini na Afrika Mashariki kwa jumla.

 

“Iwapo nitataka kutengeneza video kali ya kimataifa, nitamchukua mwongozaji kutoka nje na kumleta hapa Tanzania,” hivi ndivyo anavyosema.

 

Anasema kuwa ndani ya Tanzania kuna vivutio vingi anavyoamini akimchukua mwongozaji mwenye vifaa vya kutosha vya kimataifa, ataweza kutengeneza video yenye ubora.

 

“Unapomchukua mwongozaji kutoka nje na kumleta hapa, bila shaka itampa umakini mkubwa hata yeye mwenyewe, hivyo kufanya mambo makubwa zaidi ya afanyavyo akiwa huko. Hapa kwetu tuna vivutio vingi , maeneo yanayovutia kuna Lushoto, Arusha, Zanzibar, Bagamoyo na mengine yanayoweza kutumika kwa shughuli hii na ukaushangaza ulimwengu,” anasema Ben Pol.

 

Anasema kuwa bado anahisi anao wajibu wa kuutangaza utalii wa ndani kupitia kazi yake ya muziki.

 

“Nina wajibu na jukumu la kuwa balozi mzuri nyumbani kwetu. Najua labda watu wa nje wangependa kuona vitu vya nyumbani, ninapojitangaza kwamba mimi ni mwanamuziki kutoka Tanzania, hata kwenye kazi zangu waone mazingira ya nchi yangu,” anasema.

 

Je, hiyo ni sababu pekee ya uamuzi wake kufanyia kazi zake Bongo?

 

Ben Pol anaeleza kuwa, anapoona kazi zake zinatumika na kuombwa na watu wengi waishio nje ya nchi, hufarijika kwani inaonyesha inaeleweka.

 

“Najua kazi yangu inaeleweka, kwa watu wanaoijua lugha ninayoimba, hata kwa wale ambao Kiswahili kwao ni mtihani. Napokea pongezi nyingi, mfano wimbo wa ‘Jikubali’ ni kati ya kazi zangu zilizonipa umaarufu mkubwa nje ya nchi na ndiyo wimbo uliopigwa zaidi nje kuliko kazi zangu zote,” anasema Ben Pol.

 

Kuhusu usimamizi wa kazi zake Ben Pol anasema kuwa kwa sasa kuna mtu wa karibu anayemsaidia katika suala hilo. Anamtaja kuwa ni mshirika wake wa karibu na wanasaidiana katika kazi za muziki, lakini hana meneja.

 

Anabainisha kuwa kuna faida kubwa kwa msanii kuwa na usimamizi, lakini akasema bado kuna uhaba wa mameneja wa kazi za wasanii na kwamba kwa walipo sasa, wengi hawana ufahamu wa kazi zao.

Jumatano, 29 Januari 2014

HARAKATI ZA KUJIOKOA MORO



 Baadhi ya watu wakibeba chakula cha misaada kutoka kwa wasamaria wema. Picha na Juma Mtanda

MASHABIKI WANAO NG'ARA



Mashabiki watoto (walio mstari wa mbele) wakiishangilia timu yao ya Ashanti United wakati mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha na Michael Matemanga