Wazazi na walezi
wametakiwa kuwekeza katika elimu ya watoto kwa kuwa kufanya hivyo ndiyo
bima pekee bora kwa maisha yao ya baadaye na Taifa kwa jumla. Kauli hiyo
ilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister
Mhagama wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Naweza Kufikiri, Naweza
Kuzungumza.
Mashindano hayo yanashirikisha wanafunzi zaidi ya
100 kutoka shule 37 za sekondari wilayani Mufindi na lengo la kuanzishwa
ni kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri.Mhagama alisema wakati umefika kwa Watanzania
kuwekeza katika elimu ili kulikomboa Taifa kutoka katika umaskini,
ujinga na maradhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni