Serikali imeahidi kumchukulia
Shilole kufuatia kusambaa
kwa picha zake chafu zilizopigwa
wakati akitumbuiza
nchini Ubelgiji.
Akizungumza bungeni Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari
Vijana Utamaduni
na Michezo, Juma Nkamia, wakati
akijibu
hoja za wabunge baada ya kusoma
makadirio na matumizi
wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza
baraza la
sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia
“Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza
serikali itachukua
hatua na niombe mheshimiwa spika
kupitia bunge lako tufuku, kuliomba
radhi kwa upande wa
serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki
yule.
Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali
itachukua
hatua yake,” alisema Juma Nkamia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni