Kwa nini uharishe wakati ukiwa safirini?
Kuna maambukizo mengi watu hupata wakati wanaposafiri na ambayo
huleta kuharisha. Mengi ya haya maambukizo hayadhuru watu wanaoishi katika
sehemu
hizo ambazo wewe unasafiri kwani wao huenda walishaugua kabla (na sasa
wamejenga kinga). Watu pia huharisha wakati wanaposafiri kutokana na uchovu wa
safari na kubadilisha chakula.
Nitajuaje kama kuharisha kwangu ni maambukizo au ni kutokana na
sababu nyingine?
Ni vigumu kusema tofauti yake. Kama unaenda choo laini 2-3 kwa
kutwa na bila dalili nyingine zozote, kuharisha kwako sana sana huenda
haukuambukizwa na vimelea vibaya. Maambukizi haya yatafuatwa na kupata choo cha
maji maji mara nyingi. Dalili nyingine ni pamoja na kuharisha damu, homa,
maumivu ya tumbo na kichefu chefu.
Nitazuiaje kuharisha?
Kitu cha maana kabisa na rahisi ili kuzuia kuharisha ni kuosha
mikono mara kwa mara. Kufanya hivi ni muhimu sana haswa kabla ya kula chakula,
pia mara nyingi kuosha mikono mara kwa mara ni vizuri. Kwa kuwa sabuni na maji
sio ghali na hupatikana kila mara, kuna vitambaa vilivyolowekwa katika dawa za
kuulia wadudu (hufanya kazi vizuri sana) huwa ni rahisi zaidi kutumia wakati
ambapo sabuni na maji havikupatikana. Vitambaa hivi hupatikana katika maduka
mengi ya dawa, hata ya vyakula au stoo za vitu mchanganyiko huko Umarekani,
vichukue vitambaa hivi uendapo safari. Kama hujui jinsi ya kuvipata, mwulize
daktari au muuguzi wako.
Vyakula vingine ni salama zaidi. Chakula chochote au kinywaji
ambacho ni cha moto sana wakati kinapoandaliwa ni salama. Mikate, pipi pia ni
salama.
Vyakula ambavyo vina hatari ya kuleta madhara na kukufanya uwe
mgonjwa ni kama mboga mboga mbichi, saladi na vinginevyo vibichi au
vilivyopikwa na kuiva nusu kama vile samaki na nyama. Kama utaosha mikono yako
na kutumia kisu kisafi kumenya na kukata tunda, kwa kawaida ni salama. Epuka
matunda ambayo hayana kumenywa kama vile matunda damu. Vyakula vya maziwa kama
vile maziwa na jibini si salama labda kama vimesindikwa kwa ufundi (kuchemsha
kwa mvuke). Unaweza kutengeneza maziwa salama kwa kuyachemsha mpaka kuchemka na
kuyaacha yapoe. Maziwa ya pakiti (irradiated milk) ni salama kwa kunywa.
Maji yanaweza kukufanya ukawa mgonjwa pia. Kama maziwa, ukichemsha
maji yako yatakuwa safi na salama kwa kunywa. Maji yauzwayo, yaliyohifadhiwa
kwenye chupa pia kwa kawaida ni salama kwa kunywa. Vinywaji vilivyosindikwa
kwenye chupa (vyenye kutoa vipele vya hewa kama vile soda) pia ni salama kwa
kunywa. Hewa ya carbon inayotiwa katika vinywaji vilivyosindikwa pia huua
vimelea kwa kipindi cha masaa manne, hata hivyo kutia hewa hii katika bomba la
maji haifanyi maji yake kuwa salama kunywa kwani maji yaliyochanganywa hayakuwa
yamechemshwa. Ni lazima uepuke kutumia vibonge vya barafu labda viwe
vimetengenezwa na maji safi na pia wakati wa kupiga mswaki utumie maji safi na
salama.
Itakusaidia zaidi endapo utafanikiwa kuepuka vyakula vya aina
fulani kwa kuwa tumbo lako halikuvizoea japo vilizoeleka zamani.
Nifanye nini kama nitaharisha?
Kuna aina mbili za dawa za kuzuia kuharisha kwa wasafiri. Ya
kwanza ni zile dawa za kupunguza kasi ya kuharisha lakini hazitibu maambukizo
yaliyoleta kuharisha. Dawa hizi zinasaidia kupunguza dalili za ugonjwa. Dawa
zinazotumika sana zinaitwa loperamide (“Imodium”) na Bismuth
subsalicylate (“Pepto-bismol”), ambazo zote
zinapatikana maduka yote ya dawa bila ya agizo la daktari.
Dawa hizi zisitumiwe na watoto wadogo.
Pia, kuna (antibiotics) dawa zinazoua vimelea vibaya ndipo
hutibu ugonjwa. Kwa kuzitumia dawa hizi huweza kupunguza idadi ya siku za
ugonjwa.
Wakati unapoharisha maji maji ni lazima utumie (antibiotic) dawa
za kuulia vimelea vya ugonjwa ambazo daktari au muuguzi wako atakupa uchukue
safarini. Unaweza pia kutumia loperamidend Bismuth subsalicylate kuzia
kuharisha mpaka dawa ya kuulia vimelea vibaya ifanye kazi. Kama uko
taabani, una homa au unaona damu katika choo chako, ni lazima
utumie dawa ya kuulia vimelea (antibiotic) na SIO ile ya leperamide au Bismuth
subsalicylate.
VITU VYA KUKUMBUKA WAKATI WA KUSAFIRI
OSHA MIKONO, Na kama Huwezi kuosha mikono vya kutosha, hasa
kabla ya kula Basi (tumia vile vitambaa
vilivyowekwa dawa ya kuulia vimelea vibaya kama Purell au Aavanguard kama ni
rahisi zaidi kutumia) wengine huita sanitizer.
EPUKA VYAKULA HIVI.
Vibichi, au nyama, samaki, isiyoiva vizuri, maziwa ambayo
hayajachemshwa au jibini, majani ya mboga mboga. Matunda ni lazima yaandaliwe
kwa njia ya usafi, mahindi yakuchemsha na vyakula kama hivyo.
MAJI NA MAZIWA
Vinaweza kufanywa kuwa safi na salama kunywa kwa kuchemshwa na
kuacha chini vipoe.
Maji yanayouzwa katika
chupa kwa kawaida ni salama.
Kama umeenda choo laini mara moja au mbili kwa siku tumia dawa
ya kukusaidia katika dalili hizi, lakini
choo cha maji maji kabisa haswa kuchanganyika na damu, maumivu na homa, tumia
dawa ile ya kuulia vimelea vibaya (antibiotic).
DAWA ZA KUZUIA KUHARISHA
Wakati uonapo dalili:
Loperamide (“Imodium”)
Matumizi: Kunywa vidonge viwili kwa kuanzia, kisha kunywa
kidonge kimoja kila upatapo choo
(usinywe zaidi ya 8 katika masaa 24). Usiwape watoto wachanga, wadogo au ukiwa
mja mzito.
Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”)
Matumizi; Kama ni vidonge meza vidonge viwili
kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha
kupungue. Hata hivyo usinywe vidonge zaidi ya 16 katika masaa 24. Kama
unakunywa vitu vya maji maji, kunywa vijiko vya chai 6 (30 mls) kila baada ya
dakika 30 mpaka kuharisha kupungue. Usinywe vidonge zaidi ya 8 katika masaa 24.
Usiwape watoto wachanga na watoto wadogo.
kutibu Maambukizo
Antibiotic:
Daktari au muuguzi wako atakupa dawa ya antibiotic kusafiri nayo
unywe ukipatwa na kuharisha kubaya.
Hakikisha kuwa unaelewa jinsi ya kunywa dawa hizi kabla ya kuondoka katika
ofisi ya daktari au muuguzi. Majina ya dawa za antibiotic zinazotumika na
kujulikana sana ni kama Azithromycin (Zithromax), Ciproflaxacin, Levofloxacin
(Levoquin) na Fifaxaamin Na pia utaandikiwa dawa kwa mujibu wa daktari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni