TUAMINI NINI MAKANISANI
Mimi
huwa Napata wakati mgumu sana. Nikiwa kanisani nawasikiliza walimu na
wahubiri wakihubiri kuhusu mada ya MOYO, NAFSI, AKILI, MWILI na ROHO huwa nabaki kwenye sintofahamu ya maswala hayo. Maneno hayo yanabeba maana zipi au maana ngapi?
Kila
ninapowasikiliza wahubiri wakisisitiza hayo maeneo nabaki na maswali
lukuki. Kwa mfano utasikia au utasoma maandiko yanasema, …..moyo huwa
mdanganyifu….”, nimeliweka neno lako moyoni mwangu nisikutende dhambi…..
au utasikia wapendwa wakisema, ‘…….hilo ni kanisa la kiroho…..” Niko
rohoni….., huyu bwana yuko rohoni sana……., Haya ni mambo ya rohoni
sana…., Mtu wa rohoni huwaelewa watu wa rohoni…., na wengine utawasikia
wakisema kwamba, Mungu ni Roho nao wamwabuduo inawapasa kumwabudu katika
roho. Sehemu nyingine utakutana na watu wakisema, …..Mungu aiweke pema
peponi roho ya marehemu……nk, nk, nk.
Yote
hayo hunifanya nipate maswali mengi bila kupata majibu. Maswali
yafuatayo huwa yananiijia kwa sana kila siku na kupata majibu inakuwa
ngumu:
1. Moyo ni nini
2. Moyo unakaa wapi mwilini?
3. Je, Neno la Mungu huwa tunaliweka Moyoni au Akilini?
4. Mungu
Baba, Mungu Mwana, na Roho Mt wanakaa ndani yetu? Wanakaa Sehemu gani?
Wanakaa Moyoni, Rohoni, Mwilini, Akilini, Nafsini au Kichwani?
5. Je kuna aina ngapi za Moyo?
6. Roho ya ni nini?
7. Roho iko upande gani wa mwili?
8. Nafsi ni nini?
9. Nafsi inakaa wapi mwilini?
10. Mwili ni nini na uko wapi?
11. Mwanadamu ni nini?
12. Akili ni nini na ziko wapi mwilini?
13. Dhamira ni nini na inakaa wapi mwilini?
Hebu wapendwa nisaidieni kupambanua kulingana na uelewa wenu. Ninyi mwaelewaje?