Jumanne, 2 Juni 2015
MUIGIZAJI MASHUHURI JB ANAFANYA POUWA KWENYE MAIGIZO YANAYO FUNDISHA NAMNA YA...
Kutunza afya na mwili katika maisha yetu mfano mzuri utakuta anacheka,anafanya mazoezi, hutumia muda wake vizuri katika kupumzika kama baba na kuchukua muda wa kukaa na familia yake kubadilishana mawazo, hayo yote utayakuta kwenye flm zake jambo ambalo ni lakuigwa katika maisha yetu ya kila siku pale tu tunapo taka kutengeneza na kutunza akili zetu.
Afya ni hazina ya pekee inayotufanya tuishi kwa raha. Akili pia ni kitu muhimu kinachoendesha utendaji kazi wa mambo mengi katika miili yetu. Hatuwezi fanya jambo lolote la maana ikiwa hauna afya njema ndio maana ni muhimu kutunza afya zetu ili tuweze kuendelea kuishi vizuri na kuendelea kufanya shughuli za kujenga taifa.
Afya bora hujengwa na mambo kadha vikiwemo vyakula bora, ufanyaji wa mazoezi ya mwili na kuishi katika mazingira safi na tulivu kwa maisha ya mwanadamu.
Kwa kulijua hilo soma mambo yafuatayo yatakayokusaidia kutunza afya yako...
1. Kula vyakula bora.
-Chakula ni dawa, ni vyema ukawa daktari wa mwili wako kwa kula vyema na kuwa mwenye afya bora na imara. Kila siku jitahidi kula chakula chenye virutubisho vingi vya vyakula tofauti tofauti (Live smart by eating a well balanced diet). Kula wanga na protini kiasi, mboga za majani na matunda kwa wingi.
2. Kunywa maji mengi ( kiasi cha lita 2 kwa siku ).
-Maji ni kinywaji chenye faida kubwa mwilini, kunywa maji kila unapofanya kazi. Kujua mengi kuhusu manufaa ya maji mwilini BONYEZA HAPA kusoma makala yangu niliyokwishawahi kuandika kuhusu sababu za maji kuwa ni muhimu kwa afya yako.
3. Pumzisha mwili wako.
-Lala kila unapojisikia usingizi hata kama ni mchana, watu wengi hufikiri kulala mchana ni uvivu HAPANA, kama una nafasi sinzia kwenye kochi angalau kwa dakika 10 kisha endelea na kazi zako. Jipumzishe ili kuupa mwili wako muda wa kukusanya nguvu tena. Wewe sio dubwana (robot) ufanye kazi bila kupumzika, pumzika na ufute pumzi kwa afya.
4. Fanya mazoezi ya viungo.
-Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako, hata kama upo busy kiasi gani tafuta angalau dakika 20-30 kwa siku ufanye mazoezi iwe asubuhi au jioni. Mazoezi huondoa sumu mwilini kama hewa chafu, sumu itokanayo na vyakula tunavyokula na pia kwa kufanya mazoezi utaweka viungo vyako vizuri na kuviimaarisha. Angalia hii video hapa chini inaonyesha namna ya kufanya mazoezi nyumbani kwako bila kutumia vifaa vyovyote.
5. Penda kuchemsha bongo.
-Watu wengi hutamani kuwa ‘’GENIUS’’, ukitaka kuwa genius jijengee tabia kila siku ya kusoma mambo mengi tofauti tofauti ili uongeze uwezo wako wa maarifa (general knowledge). Soma kitu kipya kila siku kama mambo ya sayansi na teknolojia, jiografia ya ulimwengu, historia, lugha au mazingira yanayokuzunguka. Pia kula vyakula vya kuchangamsha ubongo na kuongeza uwezo wako wa kuhifadhi kumbukumbu kama njugu mawe, samaki wa kuchemsha (omega-3 amino acids), parachichi, maboga, karanga nakadhalika.
6. Cheza, imba au sikiliza music kila utakapojihisi umechoka. (RELAX!...)
-Mimi ni mpenzi wa R n B na rap wewe je? Amini usiamini muziki unaondoa stress kama unavyoongalia au kusikiliza vichekesho yani comedy. Nakushauri usikilize muziki, uimbe au kucheza kila unapohisi umechoka au umetingwa na mawazo mengi. Unajua ni kwanini kuna muda unatakiwa kujisahaulisha mambo yaliyo kichwani kwako kwa ku RELAX!!!...? ni kwasababu kichwa chako kinauwezo wa kubeba mambo mengi sana kuliko unavyofikiri. Jinsi unavyozidi kuongeza mambo kwa kufikiri matatizo yako ndipo unapozidi kuongeza msongo wa mawazo.
7. Kunywa chai kuchangamsha mwili.
-Chai huchangamsha ubongo na kufanya akili yako kuwa hai na kuongeza wepesi wa kufikiri kwa muda huo. Napendelea kunywa chai ya kijani (green tea) kuliko chai nyeusi (black tea), kujua kwanini nasema hivyo BONYEZA HAPA usome makala yangu niliyowahi kuandika kuhusu faida za kunywa chai ya kijani dhidi ya chai nyeusi.
8. Kama wewe ni mnywaji pombe, jitahidi kunywa kiasi au kuacha kabisa.
-Starehe na kwa afya ni kunywa chupa 1 hadi 2 basi, zaidi ya hapo ni kujitafutia matatizo. Watalaamu wameeleza kunywa pombe kiasi kuna faida zake ambazo ni chache lakini utakapo kunywa pombe kupita kiasi hasara ni nyingi zikiwemo kukumbwa na matatizo ya kupoteza kumbukumbu, saratani za ini, koo, matiti, maradhi ya moyo na mengine mengi.
9. Jitahidi kukaa kwenye mazingira safi na tulivu. (hewa safi ni muhimu sana)
-Moja ya tatizo kubwa la miji mikubwa hapa nchini ni uchafuzi wa mazingira. Sisi binadamu hutegemea mazingira safi kwa maisha yetu, kama nyumbani kwako au kwenu hakuna miti basi ni vyema ukapanda ili mpate hewa safi na kivuli. Uwapo ofisini, nyumbani au sehemu yeyote ambamo hakuna uwazi mkubwa wa kupitisha hewa fungua madirisha ili uruhusu hewa safi kuingia ndani. Kama kuna kiyoyozi (air conditioner) unaweza ukawasha pia ili mradi tu upumue vizuri.
10. Cheka na kufurahi angalau mara kadhaa kwa siku.
-Hakuna kitu kinachotumaliza vibaya sisi wenyewe ndani kwa ndani kama HASIRA, KINYONGO, UNYONGE na KIBURI kwa kununa. Kuwa na jazba hakutatui tatizo lolote, furahi pale unapofurahishwa na cheka pale unapochekeshwa. Kucheka na kufurahi ni tiba ya msongo wa mawazo kwasababu huchangamsha na kusawazisha akili
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni