Jumanne, 9 Juni 2015
SIKIA ALICHO KISEMA NISHER BYBEE "Mijitu mingine mnakua ..." AMBAE NI >>> Director / Producer / Recording Artist / Musician / Actor / Recording Engineer
Kula vizuri, Vaa Pendeza, Ishi unavyo taka (usivunje sheria za nchi), Nunua unachopenda, Mwisho wa siku Furahi!!! Hayo ndo maisha... Mijitu mingine mnakua na Streeeeeeessssss kisa mwenzako Anaishi vizuri, hayo sio maisha, hizo ni Njaa!
Jumapili, 7 Juni 2015
FANYA HII VII ILI KUZUIA KUHARISHA UNAPOKUWA SAFARINI>>> Maji yanaweza kukufanya ukawa mgonjwa pia*** http://baragumuhabari.blogspot.com/
Kwa nini uharishe wakati ukiwa safirini?
Kuna maambukizo mengi watu hupata wakati wanaposafiri na ambayo
huleta kuharisha. Mengi ya haya maambukizo hayadhuru watu wanaoishi katika
sehemu
hizo ambazo wewe unasafiri kwani wao huenda walishaugua kabla (na sasa
wamejenga kinga). Watu pia huharisha wakati wanaposafiri kutokana na uchovu wa
safari na kubadilisha chakula.
Nitajuaje kama kuharisha kwangu ni maambukizo au ni kutokana na
sababu nyingine?
Ni vigumu kusema tofauti yake. Kama unaenda choo laini 2-3 kwa
kutwa na bila dalili nyingine zozote, kuharisha kwako sana sana huenda
haukuambukizwa na vimelea vibaya. Maambukizi haya yatafuatwa na kupata choo cha
maji maji mara nyingi. Dalili nyingine ni pamoja na kuharisha damu, homa,
maumivu ya tumbo na kichefu chefu.
Nitazuiaje kuharisha?
Kitu cha maana kabisa na rahisi ili kuzuia kuharisha ni kuosha
mikono mara kwa mara. Kufanya hivi ni muhimu sana haswa kabla ya kula chakula,
pia mara nyingi kuosha mikono mara kwa mara ni vizuri. Kwa kuwa sabuni na maji
sio ghali na hupatikana kila mara, kuna vitambaa vilivyolowekwa katika dawa za
kuulia wadudu (hufanya kazi vizuri sana) huwa ni rahisi zaidi kutumia wakati
ambapo sabuni na maji havikupatikana. Vitambaa hivi hupatikana katika maduka
mengi ya dawa, hata ya vyakula au stoo za vitu mchanganyiko huko Umarekani,
vichukue vitambaa hivi uendapo safari. Kama hujui jinsi ya kuvipata, mwulize
daktari au muuguzi wako.
Vyakula vingine ni salama zaidi. Chakula chochote au kinywaji
ambacho ni cha moto sana wakati kinapoandaliwa ni salama. Mikate, pipi pia ni
salama.
Vyakula ambavyo vina hatari ya kuleta madhara na kukufanya uwe
mgonjwa ni kama mboga mboga mbichi, saladi na vinginevyo vibichi au
vilivyopikwa na kuiva nusu kama vile samaki na nyama. Kama utaosha mikono yako
na kutumia kisu kisafi kumenya na kukata tunda, kwa kawaida ni salama. Epuka
matunda ambayo hayana kumenywa kama vile matunda damu. Vyakula vya maziwa kama
vile maziwa na jibini si salama labda kama vimesindikwa kwa ufundi (kuchemsha
kwa mvuke). Unaweza kutengeneza maziwa salama kwa kuyachemsha mpaka kuchemka na
kuyaacha yapoe. Maziwa ya pakiti (irradiated milk) ni salama kwa kunywa.
Maji yanaweza kukufanya ukawa mgonjwa pia. Kama maziwa, ukichemsha
maji yako yatakuwa safi na salama kwa kunywa. Maji yauzwayo, yaliyohifadhiwa
kwenye chupa pia kwa kawaida ni salama kwa kunywa. Vinywaji vilivyosindikwa
kwenye chupa (vyenye kutoa vipele vya hewa kama vile soda) pia ni salama kwa
kunywa. Hewa ya carbon inayotiwa katika vinywaji vilivyosindikwa pia huua
vimelea kwa kipindi cha masaa manne, hata hivyo kutia hewa hii katika bomba la
maji haifanyi maji yake kuwa salama kunywa kwani maji yaliyochanganywa hayakuwa
yamechemshwa. Ni lazima uepuke kutumia vibonge vya barafu labda viwe
vimetengenezwa na maji safi na pia wakati wa kupiga mswaki utumie maji safi na
salama.
Itakusaidia zaidi endapo utafanikiwa kuepuka vyakula vya aina
fulani kwa kuwa tumbo lako halikuvizoea japo vilizoeleka zamani.
Nifanye nini kama nitaharisha?
Kuna aina mbili za dawa za kuzuia kuharisha kwa wasafiri. Ya
kwanza ni zile dawa za kupunguza kasi ya kuharisha lakini hazitibu maambukizo
yaliyoleta kuharisha. Dawa hizi zinasaidia kupunguza dalili za ugonjwa. Dawa
zinazotumika sana zinaitwa loperamide (“Imodium”) na Bismuth
subsalicylate (“Pepto-bismol”), ambazo zote
zinapatikana maduka yote ya dawa bila ya agizo la daktari.
Dawa hizi zisitumiwe na watoto wadogo.
Pia, kuna (antibiotics) dawa zinazoua vimelea vibaya ndipo
hutibu ugonjwa. Kwa kuzitumia dawa hizi huweza kupunguza idadi ya siku za
ugonjwa.
Wakati unapoharisha maji maji ni lazima utumie (antibiotic) dawa
za kuulia vimelea vya ugonjwa ambazo daktari au muuguzi wako atakupa uchukue
safarini. Unaweza pia kutumia loperamidend Bismuth subsalicylate kuzia
kuharisha mpaka dawa ya kuulia vimelea vibaya ifanye kazi. Kama uko
taabani, una homa au unaona damu katika choo chako, ni lazima
utumie dawa ya kuulia vimelea (antibiotic) na SIO ile ya leperamide au Bismuth
subsalicylate.
VITU VYA KUKUMBUKA WAKATI WA KUSAFIRI
OSHA MIKONO, Na kama Huwezi kuosha mikono vya kutosha, hasa
kabla ya kula Basi (tumia vile vitambaa
vilivyowekwa dawa ya kuulia vimelea vibaya kama Purell au Aavanguard kama ni
rahisi zaidi kutumia) wengine huita sanitizer.
EPUKA VYAKULA HIVI.
Vibichi, au nyama, samaki, isiyoiva vizuri, maziwa ambayo
hayajachemshwa au jibini, majani ya mboga mboga. Matunda ni lazima yaandaliwe
kwa njia ya usafi, mahindi yakuchemsha na vyakula kama hivyo.
MAJI NA MAZIWA
Vinaweza kufanywa kuwa safi na salama kunywa kwa kuchemshwa na
kuacha chini vipoe.
Maji yanayouzwa katika
chupa kwa kawaida ni salama.
Kama umeenda choo laini mara moja au mbili kwa siku tumia dawa
ya kukusaidia katika dalili hizi, lakini
choo cha maji maji kabisa haswa kuchanganyika na damu, maumivu na homa, tumia
dawa ile ya kuulia vimelea vibaya (antibiotic).
DAWA ZA KUZUIA KUHARISHA
Wakati uonapo dalili:
Loperamide (“Imodium”)
Matumizi: Kunywa vidonge viwili kwa kuanzia, kisha kunywa
kidonge kimoja kila upatapo choo
(usinywe zaidi ya 8 katika masaa 24). Usiwape watoto wachanga, wadogo au ukiwa
mja mzito.
Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”)
Matumizi; Kama ni vidonge meza vidonge viwili
kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha
kupungue. Hata hivyo usinywe vidonge zaidi ya 16 katika masaa 24. Kama
unakunywa vitu vya maji maji, kunywa vijiko vya chai 6 (30 mls) kila baada ya
dakika 30 mpaka kuharisha kupungue. Usinywe vidonge zaidi ya 8 katika masaa 24.
Usiwape watoto wachanga na watoto wadogo.
kutibu Maambukizo
Antibiotic:
Daktari au muuguzi wako atakupa dawa ya antibiotic kusafiri nayo
unywe ukipatwa na kuharisha kubaya.
Hakikisha kuwa unaelewa jinsi ya kunywa dawa hizi kabla ya kuondoka katika
ofisi ya daktari au muuguzi. Majina ya dawa za antibiotic zinazotumika na
kujulikana sana ni kama Azithromycin (Zithromax), Ciproflaxacin, Levofloxacin
(Levoquin) na Fifaxaamin Na pia utaandikiwa dawa kwa mujibu wa daktari.
Ijumaa, 5 Juni 2015
CHEKI HAPA ALICHO KISEMA A.Y KUHUSU MKOA WA NJOMBE... MWANA FA NAE KAJIPANGA KUFANYA ANACHOKIJUA
Nani
anakuja leo kwenye show yangu pale Club Vibe, Mbeya na kesho Jumamosi
pale Club Vegas, Njombe? Njoo mtu wangu tukutane, tujuane na tupige
mapicha kibao ya kuwalingishia washkaji hapa Facebook na Instagram!
Jumatano, 3 Juni 2015
HUJAWAHI JIULIZA KWA NINI WATOTO WA MJINI DAR WANAONGEA KICHIZI NA WANAJIAMINI SOMA HAPA UTAJIFUNZA KITU>>> Hii inatakiwa kuigwa na watu wa mikoani
Namna ya
kufanya:
Utahitaji;
1.
Nazi. Yaweza kuwa nazi, mafuta ya nazi, tui la nazi, dafu n.k.
2.
Chai mbichi isiyokaushwa.
3.
Vyakula - mchanganyiko wa nafaka.
Nazi imewahi
kuthibitishwa kuwa na vitu muhimu vinavyoua virusi. Lauric Acid ndiyo acid
pekee kwa kuua virusi ambayo inapatikana toka katika nazi na pengine ni toka
kwenye maziwa ya mamaake binadamu tu duniani kote.
Je,
Ni kweli Nazi inarutubisha afya?
Acid hii
ndiyo kitu pekee chenye uwezo wa kuua virusi na ni rahisi kugundua hilo kama
utakuwa mtu mwenye kumbukumbu basi nakupa Uthibitisho katika maeneo matatu.
Linganisha
afya mbovu za awali za watu waliohamia Dar Es Salaam kama vile wasichana wa
kazi za ndani, vijana wanaokuja kusoma au kuutafuta maisha n.k. wakitokea sehemu
zisipopatikana nazi.
Utamkuta mtu anakuwa hajiamini, haongei sana, mwoga, ngozi
yake imejikunja-kunja, miguu imepasuka na pengine hata kitambi cha kwashakoo ni
kawaida kwao.
Halafu angalia afya zao pale walipokula vyakula vilivyoungwa nazi
kwa muda mfupi tu kama miezi mitatu tu wakiwa hapa Dar Es Salaam.
Utagundua
kuwa afya zao zilibadilika sana.Wananenepa, Mipasuko kwenye miguu inaondoka,
Ngozi zinakuwa nyororo, kwashakoo inaondoka, wanakuwa sio waoga tena, wanaongea
sana tena kwa kujiamini na kwa kusema yote ni kuwa wanachangamka kiafya.
Kwa
wale tuliosoma “Old schools” mtakumbuka tulisoma vitabu vingi vikiwemo Alfu
lela Ulela ambavyo vilijumuisha Safari saba za Sindbad Baharia.
Katika safari
zake aliwahi kutekwa akiwa na wenzie saba baada ya chombo chao kugonga mwamba
na kuvunjika.
Watekaji waliwafungia ndani na kuwalisha “wali ulioungwa
nazi” ili wanenepe kisha wawachinje! Sindbad kwa kujua hilo
hakula kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi wenzie walinenepa sana na
walichinjwa wakaliwa! Yeye alikuwa akikonda siku baada ya siku na kuwafanya
maharamia hao kumfungulia atembee tembee awe huru ili aimarike kiafya na ndipo
alipopata mwanya wa kutoroka….
Uthibitisho
wa mwisho ni pale mtoto mchanga anapofiwa na mama yake basi huwa anaikosa
lauric acid toka ziwa la mama na afya yake nadhani wote mmeshuhudia
inavyoathirika.
Kifupi ni kuwa anatakiwa pamoja na maziwa ya wanyama
anayolishwa inatakiwa apate walau kijiko kimoja cha tui la nazi kila siku ili
kuilinda afya yake isiporomoke.
Hivyo kama
wewe ni muathirika wa maradhi ya aina yoyote, basi tumia dawa za hospitali,
halafu ili kuthibitisha hili jaribu kula vyakula vilivyoungwa nazi kwa kiasi
kikubwa, au chakula kilichokaangwa kwa mafuta ya nazi, au jenga mazoea ya
kutafuna nazi mbichi na pengine ni vizuri zaidi ukaacha tabia ya kunywa soda na
kuanza kunywa maji ya madafu pale unaposikia kiu.
Je Nazi
yoyote inatibu?
Kama kawaida
ya uhusiano wa mmea na udongo ulivyo, zipo nazi ambazo ukizipeleka katika
maabara utazikuta zina kiwango kikubwa cha lauric acid au ukakuta lauric acid
ipo kidogo au pengine ukakuta nazi haina kabisa lauric acid kwa vile udongo
ulipooteshwa nazi kuna kemikali ambazo zinasababisha udongo huo kuwa sio sahihi
kuzalisha acid hiyo katika nazi.
Pia mpaka sasa yapo makampuni ya
kusindika nazi ambayo yanakamua nazi zenye lauric acid ya kutosha na kuuza kama
dawa.
Nazi hizo zimeingizwa nchini na ninazitumia kutoa tiba kwa waathirika na
hakika zinapunguza idadi ya watu wenye afya mbovu.
Lakini mpaka sasa hakuna
taarifa zilizowafikia wawekezaji wa ndani hasa katika sekta ya afya ambao
ningeweza kushirikiana nao kuitafiti bidhaa hii nchini watu wale na wapone.
Je, Nazi
zinapatikana?
Upande wa
pili wa shilingi una sura ya nazi kuwa bidhaa ya wenye nazo tu mara baada ya
habari hii kuenea.
Sasa Vile vile ni vema kwa wizara za kilimo na chakula
pamoja na wizara ya afya kukaa chini na kuangalia namna ya kukabiliana na
changamoto hii ya kupungua kwa nazi masokoni pamoja na kupanda kwa bei ya
bidhaa hiyo ambayo inaweza kufikia shilingi elfu tatu kwa nazi moja endapo theluthi
moja tu ya watanzania wataamua kuitumia nazi kama dawa ya kurutubisha afya zao.
Wakati
naendelea kukuletea habari hii, ni vema ukaituma email hii kwa watu ishirini au
wote katika address book yako ili tupunguze idadi ya watu wenye matatizo ya kiafya.
Tusifiche tiba maana kuwa na taifa lenye wagonjwa ni UMASIKINI. Tafadhali tuma
sasa.
Jumanne, 2 Juni 2015
KWA MARA YA KWANZA OMMY DIMPOZ KAF...
Afanana na jamaa ambae ukimcheki tuu unaweza ukadhani ndo munene mwenyewe ama ni nduguye Ommy Dimpoz mcheki hapo chini
Kwa mara ya kwanza mimi binafsi nilidhani ni Dimpozi mwenyewe au macho yangu tuu ndo dhani hata wewe utakuwa shahidi angalia kwa makini na utajua duniani ni wawili wawiliii.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)