Alhamisi, 21 Juni 2018

WANAKIJIJI WAUZA FIGO KWA SABABU YA HALI DUNI KIUCHUMI



kuna hii ya kuifahamu kuhusu Kijiji cha Hokse nchini Nepal kimebatizwa jina jipya la ‘Kidney Village’ baada ya Watu karibia wote wanaoishi kwenye kijiji hicho kuwa wameuza Figo zao.
 
Inadaiwa kuwa Wakazi wa Kijiji hicho hali zao za kiuchumi ni duni sana kitu kinachowasukuma kuingia katika biashara ya kuuza Figo zao ili wapate fedha za kujikimu mahitaji yao.

Mkazi mmoja aliyetambulika kwa jina la Geeta mwenye miaka 37 alisema kuwa yeye na Mume wake walisafiri mpaka kwenye Hospitali moja huko nchini India ili kutolewa Figo zao na kulipwa  zaidi ya shilingi Milioni 3 za Kitanzania.

Aidha familia hiyo ilitumia fedha hizo kununua kiwanja na kujenga nyumba yao na isivyo bahati nyumba hiyo iliangushwa na tetemeko la ardhi lililotokea kijijini hapo.

Kwa upande mwingine madalali wanaofanya biashara hiyo ya figo wametajwa kuzunguka sana katika kijiji hicho na kuwashawishi Wanakijiji hao kuuza Figo zao.

Jumatano, 9 Mei 2018

MVUA KUBWA ITAKUJA KWA SIKU TANO MFULULIZO #TMA

See the source image
Mvua kubwa yatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Utabiri huo umetolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini (TMA), ambao umeeleza kuwa kiwango hicho cha mvua kilitarajiwa kuanza jana usiku.

Kwa mujibu wa utabiri huo kiwango cha mvua hiyo kitaendelea kwa siku tano hasa wanaoishi mabondeni, wametakiwa kuchukua tahadhari.

TMA imeeleza kwamba athari zinazoweza kutokea ni mafuriko ambayo yatasababisha msongamano wa magari na watu hali itakayochelewesha usafiri na usafishwaji maeneno ya mjini.

Aidha kwa siku ya jana asubuhi kulikuwa na wingu zito lililoashirijia ujio wa mvua kubwa, lakini haikunyesha mvua hiyo kama ilivyotarajiwa huku asubuhi ya leo majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam imenyesha mvua ambayo imedumu kwa kipindi kifupi.

Jumanne, 8 Mei 2018

CHUI ALIYEMLA MTOTO WA MIAKA MITATU NCHINI UGANDA ATAFUTWA

See the source image

Maafisa wa nyama pori nchini Uganda bado wanamsaka Chui aliyemla mtoto wa miaka mitatu

8.5.218 KUNAUWEZEKANO WA KUFUTWA KWA KESI YA MKURUGENZI WA SHULE YA LUCK VICENT

Mahakama ya Wilaya ya Arumeru imetishia kuifuta kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vicent na wenzake kwa sababu ya upande wa mashtaka kuomba kesi hiyo iahirishwe mara kwa mara.
Hayo yamesemwa na Hakimu wa mahakama hiyo, Desderi Kamugisha baada ya wakili wa serikali, Alice Mtenga kuomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine ili waifanyie mabadiliko hati ya mashtaka.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Wakili wa utetezi, Method Kimomogolo alikubaliana na hoja za wakili wa serikali, kwamba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Hakimu Kamugisha alikubaliana na ombi la ahirisho la kesi hiyo, huku akiuonya upande wa mashtaka kwamba kama haujajipanga vizuri kuhusu kesi hiyo anaweza kuifuta kwa sababu inaahirishwa mara kwa mara.
Baada ya kusema hayo aliahirisha kesi hiyo hadi May 8, 2018 kwa ajili ya kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.

8.5.2018 NCHINI HAWAII WANANCHI WAMEONDOLEWA MAJUMBANI MWAO



a fire in a field: Lava flows across a yard in the Leilani Estates neighborhood of Pahoa, Hawaii on May 6, 2018.
Watu zaidi ya 1700 wameondolewa katika nyumba zao katika eneo Kilauea nchini Hawaii kutokana na tope la volkano.
Wakazi wa eneo ambalo limekumbwa na volkano wameondolewa wakihofiwa kudhurika kutokana na moshi wa tope la volkano na kupelekwa katika eneo salama.

Tope hilo la volkano linatoa moshi ambao wanasayansi wamesema kuwa ni hatari kwa maisha ya binadamu.

VIMINI VYA ZUILIWA ILI KUPUNGUZA WANAUME KUFELI

See the source image
Maktaba ya chuo kikuu nchini Zambia imepiga marufuku wanafunzi wa kike kuingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamevaa vimini kwakuwa wanawachanganya wanafunzi wa kiume wakiwa wanasoma.
Chuo Kikuu cha Zambia iliyopo katika jiji la Lusaka imeweka tangazo maalum kuzunguka maktaba yake hiyo kubwa kuwataka wanafunzi wa kike kuvaa mavazi ya heshima.

Wanafunzi wa chuo hicho chenye jina kubwa barani Afrika wanasifika kwa kuvalia mavazi ‘yanayokwenda na wakati’, wakichukua mitindo ya watu maarufu zaidi kwenye ulimwengu wa muziki na uigizaji.


“Tumebaini kuwa wanafunzi wengi wa kike wanaingia maktaba wakiwa wamevaa nusu uchi, hali inayowachanganya wanafunzi wa kiume,” tangazo hilo limeeleza.
“Kwahiyo, tunawataka wanafunzi wa kike kuvaa mavazi ya heshima wanapokuwa wanatumia maktaba. Mavazi ya heshima ndio njia ya kwenda nayo,” linasomeka zaidi tangazo hilo.

Hata hivyo, tangazo hilo limepata mapingamizi kutoka kwa wanafunzi wa kike ambao wamedai wanafunzi wa kiume hawawezi kuchanganywa na miguu kama wameamua kwenda kusoma.

Jumatatu, 7 Mei 2018

ALI KIBA AFUNGULIWA KESI KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU KISA MTOTO

See the source image
Mfanyabiashara wa nguo za mitumba jijini Dar es Salaam, Hadija Hassan amefungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akimlalamikia Ali Saleh Kiba, maafuru kama Ali Kiba kwa kutotoa matunzo ya mtoto aliyezaa naye.
Kupitia hati ya Mashtaka, mlalamikaji amedai kuwa alijifungua mtoto huyo aliyezaa na Ali Kiba mwaka 2013 katika hospitali ya Mikocheni jijini Dar es Salaam na kwamba hadi sasa mtoto huyo hapati matunzo muhimu kutoka kwa baba yake.
Hadija anaiomba Mahakama kuamuru Ali Kiba awe analipa kiasi cha sh 1.41 milioni kwa mujibu wa sheria, akirejea sheria ya watoto ya mwaka 2009.
Akielezea mgawanyo wa kiwango hicho cha fedha, alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, “Ali Kiba anapaswa kutoa huduma kila mwezi, chakula sh 150,000, matunda sh 50,000, chakula cha ziada sh. 50,000, michezo na burudani za watoto sh. 100,000, nguo sh. 60,000 na matibabu shilingi 50,000.”

Jumapili, 6 Mei 2018

ITAMBUE HAIBA YAKO (Know your Personality)

See the source image
Katika utafiti wakuchunguza athari za msongo wa mawazo katika moyo, madaktari Mayer Friedman na Ray Roseman waliweza kuwaweka watu katika makundi ya haiba mbili; yaani haiba kundi A and haiba kundi B.
Madaktari hawa waligundua kuwa hata kama kazi na aina ya maisha ingefanana, watu wa haiba kundi A wangekuwa na nafasi mara 3 kuteseka na msongo wa mawazo, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu n.k. na watu hawa mara nyingi huwa wanamaudhi kwa jinsi wanavyojibu au kuongea na wengine, na hili limekuwa likiwaongezea msongo wa mawazo maradufu.
Makundi haya yamewekwa ili kukuwezesha wewe kujua uko upande gani. Usichanganyikiwe wala kushtuka pale utakapojikuta una tabia za makundi yote mawili, mara nyingine inaamaanisha kuwa uko vizuri katika kuhakikisha mambo yanafanyika inavyotakiwa au unavyotaka yawe. Ila kama unajikuta unatabia zaidi ya nusu za haiba kundi A inabidi uchukue uamuzi wa kutafuta kubadilika au kubalisha mtazamo ulionao katika maisha, kabla haujajihatarishia maisha yako wewe mwenyewe.
Haiba Aina ‘A’
– Ni watu wa ushindani katika kila kitu wafanyacho.
– Watu wenye haiba ya kutumia nguvu na kulazimishisha
– Hufanya mambo yao mengi kwa haraka
– Huwa na uchu wa kupandishwa vyeo na kujulikana katika jamii. (Hatakama hawana sifa).
– Hutaka sana kujulikana na kuheshimiwa kwa kile walichokifanya.
– Hukasirishwa kwa haraka na watu au matukio fulani
– Huongea mara kwa mara kwa kufoka au kwa vitisho
– Hupenda kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
– Hutembea na hata kula kwa haraka
– Mara nyingi kuchukizwa sana pale wanapocheleweshwa
– Hujali sana muda na kukazana kumaliza mambo kwa muda ulipangwa (meating deadlines)
– Kila mahali huwepo kwa wakati na kwa muda muafaka.
– Mara kwa mara misuli yao ya uso huonyesha, kumaanisha, kuogopesha au ukali,
Haiba Aina ‘B’
– Sio watu wa ushindani mfano, makazini, michezoni, masomoni n.k.
– Ni watu walio rahisi, na huyakubali mazingira, hufanya vitu taratibu na kwa kufuata kanuni.
– Huendelea na kuchukuliana na hali ya kazi iliyopo.
– Huridhika na nafasi walinayo katika kijamii.
– Hawahitaji kujulikana au kutambulika katika jamii au hata katika matukio.
– Sio rahisi sana kuwaudhi.
– Mara nyingi hufurahia sana wanapokuwa pekeyao.
– Ni wavumilivu.
– Hupendelea kufanyakitu kimoja kwa muda muafaka kabla ya kwenda kwenye kitu kingine.
– Hutembea, na kula kwa nafasi na utulivu.
– Hawakimbizwi sana na muda, sio wakukimbizana sana na kumaliza kazi.
– Mara nyingi ni wachelewaji.
– Nyuso zao ni za kufurahi na sio za mikunjo.
KWANINI UKO VILE ULIVYO?
Vyovyote haiba yako ilivyo na kwa vyovyote unavyowachukulia wale wenye tabia ngumu fahamu kuwa mfano huo ulishakuwepo miaka mingi iliyopita, labda zaidi ukiwa mtoto ndio ilikuwa chanzo cha vile ulivyo leo; Mwanasaikolojia mmoja aliuita mfumo huu “A child is a father of a man” yaani
Mambo tunayoyaona au unayoyaona kwa mtoto hutupa picha halisi ya ukumbwa wake utakavyokuwa. Zaidi ya asilimia sitini ya yote yanayoendelea maishani mwetu leo yanachangiwa na makuzi yetu tukiwa watoto. Wengi wetu tumejiharibia misingi yetu ya uwezo wa kuishi na watu wenye tabia ngumu na hivyo kujikuta tunaumizwa tokea tukiwa watoto wadodo. Habari njema ni kwamba hakuna ulazima wa kubaki vile ulivyo, mabadilko yanawezakana, inawekana katika hatua yoyote kubadili mtazamo au muonekano wako na kuboresha ujasiri wako.
Tujaribu kuangalia baadhi ya sababu zinazosababisha mtu kujiona au kujitazama vibaya, hii itakuwezesha wewe kujua uko wapi na kwanini.

1. Watu wa kwanza kabisa waliowahi kuwa karibu na wewe ni baba na mama yako au yoyote aliyechukua nafasi yao, mfano mlezi, babu, bibi nk. Kutokana na mtazamo wao juu yako, hapo wewe umetengeneza au kuzalisha mtazamo juu yako mwenywe najinsi unavyojithamini au kutojithamini. Kwa lugha rahisi ni kwamba, jinsi unavyojiangalia ulivyo leo kunatokana kwa kiasi kikubwa na jinsi wao walivyokuwa wanakutazama, kama walikuona wewe lofa na mjinga basi kuna uwezekano mkubwa na wewe leo utajiona lofa tu.
Najua wapo wazazi wasio na hekima wala wema kwa watoto wao, huwasababishia watoto wao majeraha ya kimwili, kihisia na hata kiakili, uzuri ni kwamba fungu la wazazi hawa ni dogo. Ingawa inawezekana sana kwa wazazi au walezi au watu wazima wowote kusababisha majeraha na athari kwa watoto mara nyingine pasipo kujua kwamba wanafanya hivyo. Katika kuongea na wazazi lukuki nimegundua kwamba asilimia kubwa ya watoto wameharibiwa na wazazi wao wenyewe, pasipo wazazi hawa kujua kuwa wanawaharibu watoto wao.
2. Wazazi ambao huwalinda na kuwatetea sana watoto wao, wakijaribu kuwafanyia kila kitu kwa niaba ya watoto hao, kwa njia hii wazazi hawa hutengeneza watu wazima (wababa au wamama) wenye utegemezi mkubwa, wasioweza kufanya kitu chochote wenyewe wala kusimama kwa miguu yao wenyewe. Unakuta hata kazi za shuleni mama ndiyo anafanya, mtoto anakuwa hata kuosha mwili wake hajui, na hawa ndio wale ambao ndoa huwashinda mapemaaa.
3. Wale wazazi au walezi ambao hutoa mahitaji kwa watoto wao lakini hushindwa kuonyesha kwa matendo upendo wao kwa watoto wao (mfano. Kuongea nao, kucheka nao, kucheza nao n.k.) hutengeneza kizazi kinachoamini kuwa hakipendeki, hakina mvuto, kisicho na thamani na kisichostahili kupendwa. Baba haijalishi unatoa mahitaji yote yanayohitajika nyumbani kwako, hilo sio pekee watoto wako wanalolihitaji kutoka kwako, wape muda wakuwa pamoja nao, waruhuru kucheza na wewe kidogo, toka pamoja nao, jibu baadhi ya maswali yao, waruhusu kujuwa kumbe baba au mama anaweza kuwakaribu na sisi pia.
4. Wazazi au walezi ambao kila mara humwekea mazingia mtoto kujiona aliyeshindwa, kila wakati ni wakufeli tu, wazazi hawa ni wale wanaosema kwa nini mtoto asijitahidi, kwanini asiwe wa kwanza darasani, ni mpumbavu n.k.. hali hii huharibu kabisa imani ya mtoto kwake yeye mwenyewe, huua kule kujiamini kwake na pia kutokiamini kile anachokifanya.
Yawezekana kuna vitu vilivyoonekana katika makuzi ya mtoto ambavyo hakuna wa kulaumiwa lakini bado vitu hivi huathiri sana kujiamini na kujithamini kwa mtoto yule.
Mtoto au watoto wanaohama hama au kuhamishwa shule mara kwa mara, kwa sababu zao binafsi au kwa sababu ya kuhama hama kwa wazazi hupata shida yakujiona wapweke kwa maana kila wakati hupata kazi ya kutengeneza marafiki wapya na kwamuda fulani hali hii huathiri haiba zao na kujenga kitu tunachokiita “inferiority complex”

EPUKANA NA MARADHI KWA NJIA HII



[​IMG]

Unapo amka asubuhi kula tunda la tufaha (apple) hutoweza kuonana daktari siku nzima.

kula jani la mrehani au punje 1 ya kitunguu saumu hutapata ugonjwa kansa saratani.

kunywa asubuhi juisi ya lemon asubuhi hutapata unene.

kunywa glasi 1 ya maziwa ya ng'ombe hutopatwa na maradhi ya mifupa kuuma mwilini.

kunywa maji ya uvuguvugu lita 3 kwa siku hutopatwa na maradhi yoyote yale.

Jumatano, 2 Mei 2018

KUSIMAMISHWA MASOMO MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA (TSNP), ABDUL NONDO, NI AIBU WABUNGE WA INGILIA KATI

See the source image
SUALA la Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, kusimamishwa   masomo  katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), limetua bungeni baada ya baadhi ya wabunge kuitaka Serikali kuifuta sheria inayoruhusu mwanafunzi  kusimamishwa masomo.
Uongozi wa chuo hicho  ulimsimamisha masomo Nondo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu, baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakima Mkazi Mkoa wa Iringa.
Nondo  alisimamishwa Machi 26, mwaka huu kwa barua aliyoandikiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye.
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), aliitaka Serikali kufuta sheria hiyo kwa kuwa inakiuka haki za binadamu.
Bobali  alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliyowasilishwa juzi na Profesa Joyce Ndalichako.
Alisema ni jambo la kushangaza kuona mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu  anasimamishwa  masomo baada ya kushtakiwa kwa sababu tu kanuni za uongozaji wa chuo (prospectus) zinazuia mwanafunzi husika asiendelee na chuo.
“Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, watanzania wote wana haki ya kushtaki au kushtakiwa isipokuwa rais wa Tanzania, lakini elimu ya chuo kikuu ni elimu ya ngazi ya tatu.
“Mwanafunzi huyu amepita elimu ya msingi na sekondari hadi kufikia elimu ya chuo kikuu, wanaosoma pale siyo lazima wawe vijana hata watu wazima wanasoma na wapo wengine wanaoshtakiwa.
“Sasa jambo la Nondo kuwa ameshtakiwa na kusimamishwa masomo, kama kuna sheria ya kanuni za uongozaji wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zinasema hivyo, muongozo wa namna hiyo haufai.
“Sheria hiyo inafaa ifutwe kwa sababu haiendani na wakati kwa sababu  inanyima na kuzuia haki za binadamu lakini pia inakwenda kinyume na katiba ya nchi inayotoa fursa ya mtu kushtaki na kushtakiwa.
“Nasema kwa sababu najiuliza ni kweli kati ya wanafunzi wote waliopo vyuo vikuu aliye na kesi mahakamani ni Abdul Nondo pekee? Ni kweli?
“Kama sheria za chuo zinasema hivyo  nakushauri waziri zifuteni zinawatia aibu vinginevyo mtuambie jambo hili mnalichukualia kisiasa,” alisema Bobali na kukatizwa na taarifa iliyoombwa na Mbunge wa Mgogoni (CUF), Dk. Ally Yusuf Suleiman.
Dk. Yusuf alisema: “Kama alivyosema mchangiaji kwamba ni haki ya kushtaki na kushtakiwa na bila ya kupoteza nafasi tunao wabunge wameshtakiwa mahakamani na wengine wamefungwa lakini hawajapoteza ubunge wao. Inakuwaje mwanafunzi huyu ambaye kashtakiwa tena kwa makosa ya kubambikiziwa kwa kuwa hayajathibitishwa… inakuwaje afutwe masomo?”
Hata hivyo, Mbunge huyo alikatishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ambaye alisema huo ni mchango wake na si taarifa.
“Jambo hili linakichafua Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lazima tuseme ukweli…   hadhi ya UDSM kwa sasa tunataka kukiingiza kwenye siasa.
“Ukifanya sensa ya wanafunzi wangapi wenye kesi mahakamani hawatapungua wanafunzi 20 au 30 ila aliyeonekana mwenye kosa na kunyimwa kuendelea na masomo ni mmoja tu. Hii si haki kabisa,” alisema.
Mbunge wa Mgogoni (CUF), Dk. Ally Yusuf Suleiman  alimtaka Waziri Ndalichako kubainisha   kiwango cha fedha za mikopo ya elimu ya juu kilichotengwa kwa ajili ya wanafunzi wanaotokea Zanzibar.
Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta (CCM), aliitaka Serikali kuunda bodi huru ya usimamizi wa elimu.
“Bodi hii itaangalia mitihani inayotungwa na mambo mengine muhimu ambayo yanaweza kuboresha elimu yetu.
Mbunge wa Kuteuliwa, Abdalah Bulembo aliitaka serikali kueleza imejiandaaje kuwapokea wanafunzi watakaohitimu darasa la sita na saba mwaka 2020 baada ya sera ya elimu nchini kubainisha kuwa kuanzia mwaka 2015 elimu ya msingi itakuwa miaka sita.

See the source image

RAIS Dk. John Magufuli, amesema atahakikisha kabla ya kipindi chake cha urais hakijaisha, anapandisha mishahara ya watumishi wa umma.
Amesema atapandisha mishahara kwa kiwango kinachoridhisha na si cha Sh 10,000.

Akizungumza jana wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi mkoani hapa, Rais Magufuli, alisema nyongeza ya mwaka ya mishahara itaendelea kama kawaida.

“Kwa bahati mbaya, leo Dk. Msigwa (Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi – TUCTA, Dk. Yahya Msigwa), amenichomekea kuwa Moshi niliahidi, lakini sikuahidi kwa sababu naikumbuka hotuba yangu, leo ndiyo ninaweza nikaahidi.
“Kama miradi hii itaenda vizuri na kama wafanyakazi hawa 52,000 tutawaajiri na kuwalipa misharaha vizuri na kama vyama vya wafanyakazi vitaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya awamu ya tano na hili nalizungumza vizuri na mninukuu vizuri.
“Kipindi changu cha urais hakitaisha kabla …


DOGO JANJA AFANYA MAKUBWA



Image result for dogo janja
Staa wa Bongo Flevani Dogo Janja azidi kuyaweka mapenzi yake hadharani na muigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wake ingawa wengi hadi sasa bado hawaamini kuhusiana na penzi lilopo kati yao


Kupitia ukurasa wa instagram wa Dogo Janja amepost picha akiwa na mke wake Irene Uwoya na kuandika caption yenye maneno mazito kwa mpenzi wake “thamani ya upendo wako ni ya maisha kama maisha yalivyo ni upendo”


Baada ya caption hiyo Irene Uwoya alimjibu Dogo Janja na kusema “Nakupenda leo jana na milele