Jumapili, 31 Mei 2015

ENOCK BELLA ANANYOTA KALI


Image result for yamoto band












 Kwa macho tu najua utakuwa umeshuhudia jinsi Bella alivyo na nyota ya kupendwa sijui nikutokana na sauti yake ya umahiri aliyonayo ama ni sura labda, ni vitu wanavyo jiuliza wengi juu ya jomba Bella bass ndani ya yamoto band

Hata ivyo jamaa amekuwa na njonjo nyingi katika upande wa kudansi labda nayoimekuwa sababu labda.   



Image result for yamoto band








Image result for yamoto band
Jioneee mwenyewe jinsi mshikaji anavyo jiachia, picha ni kwahisani ya HZB.

Pia kama umeicheki show waliofanya London utakuwa shaidi kuhusu namna alivyo shangiliwa na mashabiki waliokuwa wanahamu ya kuwaona wote wakianza kutumbuiza na kuporomosha nyimbo zao

UZUSHI JUU YA JUSTIN BIEBER Vs DAIMOND PLATNUMZ >.>> Ni ndege wanao ruka pamoja ingawa hawafanani hapa rangi zao soma hapa---



















Da ni fikra za kipuuzi naweza kusema ivyo kutokana na watu wanao dhani kila anaefanikiwa lazima apite kwenye ulimwengu wagiza wapo wanaozidi kusema kuwa huyu dogo anatumia ushirikina, jamani hata kama huna masikio huoni? 

Dogo anajuhudi na isitoshe anausimamizi mzuri kama alivyo leo mzee mapesa na penda kumuita billioner young super star Daimond Pltnm ambae anazidi kung'aa kwa juhudi na kujituma huku na kule lengo kutengeneza msingi mzuri hata wa wasanii wengine wadogo wanaotokea Afrika hususani Afrika mashariki.
Image result for justin bieber

Kitu kingine cha ajabu na kinacho wapajeuri wavifu wakufikiria et wanapendwa na wanawake wanapo kuwa stegini wanadai wanatumia dumba kuwavuta mmmmmmmh si kweli 













Nimeamini pesa ni mbolea kwenye mapenzi.

JIPYA KUHUSU MAAMBUKIZO KATIKA NJIA YA MKOJO




Maambukizi katika njia ya mkojo au kama unavyojulikana kwa wengi UTI huathiri mfumo wa mkojo ikiwa ni pamoja na ureter ambayo ni kama bomba linalosafirisha mkojo kutoka kwenye figo, pia kibofu cha mkojo na urethra.

 Ugonjwa huu unaathiri zaidi kibofu cha mkojo na urethra lakini unaweza pia kuathiri figo.

 Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa simple cystitis au Bladder infection, na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa pylonephritis au kidney infection. 

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli (E. coli) na tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa. 

Lakini baadhi ya watu wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi ingawa pia zipo sababu nyingine chache. 

Bakteria wa Escherichia coli hawasababishi peke yao UTI bali huambatana na wengine waitwao staphylococcus, saprophyti cus, pseudom onas, enterobacter na kadhalika.

 Maambukizi katika njia ya mkojo lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo na si pengine popote.

 Wapo wanawake ambao wamekuwa wakidhani kwamba tatizo la kutokwa na uchafu ukeni ni ugonjwa huu, na hilo si sawa kwani huo ni ugonjwa tofauti kabisa na UTI.

 Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo, inamaanisha ni kutoka eneo la nje ya utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.

 Kama maambukizi yako katika eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalamu huitwa Lower Urinary Tract Infection na yakihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.

 Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake husababishwa na kutojisafisha vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani zilizochafu.

 Pia huweza kusababishwa na matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa asili wa eneo la uke na kuwapa fursa bakteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi.

 Halikadhalika upungufu wa homoni ya wanawake iitwayo Oestrogen husababisha bakteria wanaosababisha maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi.

 Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu, unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha pia huchangia tatizo hili. 

Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.

 Sababu nyingine inayosababisha UTI ni matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha au kuoga ambayo huweza kuweka bakteria kwa urahisi na kupelekea mwanamke kupata ugonjwa huo.

 Uchafu wa vyoo umetajwa kuwa sababu nyingine, kwani matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu huweza kusababisha mwanamke kupata UTI kwa sababu ndani ya choo kuna bakteria wengi ambao wanaweza kusababisha ugonjwa huo.

&&&&&&

Matatizo haya ya maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake, huwakumba pia watoto wadogo wa kike kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi, njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani.

 Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao huweza kupata maambukizi rahisi ya UTI iwapo watajisafisha kwa kutumia maji yasiyo salama ambapo huwa rahisi kwa bakteria kubaki katika ngozi inayoning'inia (govi).

 Pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambuzi ya UTI kutokana na sababu tuliyoitaja ambapo pia ni rahisi kwao kuambukizwa Ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana tohara kwa wanaume husisitizwa.

Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo husababishwa zaidi na bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kwa kuingia na kujikita katika mfumo wa mkojo.

 Bakteria wengine wanaoleta maabukizo katika njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, trimonas na fangasi ambapo huwaathiri watu pale wanapojamiiana bila kutumia kinga na watu wenye maradhi hayo. 

Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo, mara kwa mara, ni vyema kutumia kinga na kwa mwanamke wanashauri kila wanapomaliza kufanya tendo la ndoa wakojoe ili kuondoa bakteria walioingia au waliokaa katika tundu ya mkojo wakisubiri kuingia.

 Baada ya kujua hayo yote hivi sasa tuzijadili dalili za ugonjwa wa UTI.

Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa, mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali ijapokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo.

 Dalili nyingine za UTI ni maumivu, kutokwa na usaha wakati wa kukojoa, kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi moto wakati mkojo ukitoka. 

Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.

 Wengine wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo, au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.

 Mgonjwa anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu, kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili huonesha kuchoka.

Wagonjwa wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi.

 Matatizo haya ya mfumo wa mkojo kama tulivyoona kabla huwapata watu wote wanawake na wanaume.

 Watu wenye matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI. Kwa wanaume huhisi hata nguvu za kiume kupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo la ndoa.

Kwa wajawazito ugonjwa unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni.

 Bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha madhara mengine kama vile shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji kazi mbovu wa figo.

&&&&&

Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.

 Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin, Monurol, Furadantin, Sulfam ethoxazole, co-trimax, ampicillin, gentamicin na kadhalika. 

Mgonjwa anayesumbuliwa na UTI hapaswi kutumia dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.

Wanawake wanashauriwa kuepuka kujisafisha sehemu za siri na maji machafu na yasiyo salama, pia kuepeuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pamba zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi. 

Pia wanashauriwa wanapojisafisha baada ya kujisaidia kuanzia mbele kwenda nyuma, ili kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa na kuingia njia ya mkojo. 

Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi ya UTI. 

Kwa mwanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kujipenyeza hadi katika korodani na huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kunaweza hata kusababisha mgumba. Hivyo wanashauriwa kuhakikisha wanatibu bila kuchelewa ugonjw ahuo. 

Pia maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume (prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi.

 Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.

Mpenzi msikilizaji madaktari wanatueleza kuwa, tunaweza kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi, iwapo tutawahi kabla tatizo halijawa sugu.

 Kwa maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. 

Ukinywa maji ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa. 

Katika hali ya kawaida, ugonjwa wa UTI hutoweka ndani ya siku tatu mara baada ya kuanza kutumia tiba asili ya kunywa maji mengi na juisi ya matunda halisi, iwapo ugonjwa utaendelea kuwepo baada ya siku hizo, hiyo itakuwa na maana ugonjwa wako umeshakomaa na hivyo hauwezi kutibika kwa tiba hii ya nyumbani na itakuwa inapaswa kwenda hospitalini na kuonana na daktari ambaye atafanya uchunguzi na kutoa dozi sahihi ya kutibu ugonjwa huo.



TAZAMA IYO

Ijumaa, 29 Mei 2015

UNAUJUA UKIMWI


Image result for picha za waathirika wa ukimwi

Neno Ukimwi lina maana ya Ukosefu wa Kinga Mwilini. Hapa virusi vya HIV huwa vimeshambulia kinga ya aliyeambukizwa kiasi kuwa, mwili wake wauwezi tena kujipa ulinzi dhidi ya maambukizo.

Hivyo huonyesha dalili za magonjwa tofauti tofauti na hata saratani, hapo ndipo wanasemekana kwamba wana ukimwi. Wakati huo ndipo kinga yao ya mwili huwa ni dhaifu sana, na magonjwa alo nayo yanakuwa vigumu kuyatibu na ndipo hapo ukimwi unasababisha kifo.

Fahamu kuwa kila mtu hukumbana na viini ambavyo husababisha magonjwa, lakini kama kinga yako ni imara si rahisi kupata maambukizo na hata ukipata ni rahisi kuyatibu lakini kwa wale waishio na virusi vya ukimwi kinga yao huwa imedhoofishwa sana kiasi kuwa akikumbana na viini ni rahisi kwake kupata maradhi na hata akitibiwa inachukua mda kupona.

Lakini ni vyema kufahamu kuwa siku hizi kuna dawa spesheli kwa watu wenye virusi vya HIV ambazo hupunguza makali ya ukimwi. Dawa hizi husaidia kuzuia kuzaana kwa virusi vya HIV mwilini. Hata hivyo hadi kufikia sasa kwa hakika hakuna chanjo dhidi ya virusi vya ukimwi, na hakuna dawa ya kutibu Ukimwi.

Lakini kwa jinsi matibabu yalivyoimarika katika miongo michache iliyopita, inamaanisha kwamba maisha ya baadhi ya watu walio na virusi vya Ukimwi yanaweza kurefushwa kwa miaka kadhaa.

Jinsi maambukizo ya HIV yanavyotokea.
Virusi vya HIV husambazwa kwa njia zifuatazo:
  • Kufanya ngono bila kinga.
  • Kuchangia sindano.
  • Mama aliyeambukizwa anaweza kumwambukiza mwanawe wakati wa uja uzito, kuzaa au kunyonyesha.
  • Kutangamana kwa damu au majimaji mengine ya mwili – mfano damu iliyo na virusi ikipenya kwenye jeraha au mchubuko.
  • Kuongezewa damu iliyo na virusi.
Huwezi kuambukizwa virusi kupitia:
running character by Tayo
TAYO
  • Kupigana busu, kugusana, au kuamkiana kwa mikono.
  • Kutumia kwa pamoja vifaa vya kulia chakula.
  • Kukohoa au kwenda chafya.
  • Kuumwa na wadudu kama kunguni au mbu au wanyama.
  • kupitia Vidimbwi vya kuogelea.
  • Kula chakula kilichotayarishwa na mtu aliye na virusi vya ukimwi.
Dalili za virusi vya Ukimwi?
Watu wengi walioambukizwa virusi vya HIV, huwa hawafahamu kama wameambukizwa, kwa sababu hakuna dalili zinazotokea mara moja baada ya kuambukizwa.

Watu wengine hupata homa, vipele, maumivu ya viungo na uvimbe mgumu, lakini dalili hizi zinaweza kutokea kati ya wiki sita na miezi mitatu, baada ya kuambukizwa.

Hii ni kusema mara nyingi mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi huenda asionyeshe dalili zozote, lakini tahadhari isipochukuliwa wanaweza kuwaambukiza watu virusi hivyo.

Matibabu ya kupunguza makali ya ukimwi
Bado hakuna tiba ya ukimwi, lakini kuna dawa spesheli ambazo zinaweza kusaidia waishio na virusi kwa kuimarisha afya hivyo basi kuongeza umri.

Nifanyeje kama nahisi nimeambukizwa virusi vya HIV?
Njia ya pekee ya kugundua kama una virusi vya hiv ni kwa kufanyiwa uchunguzi wa HIV.

Kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya HIV si vigumu.
Unachotakiwa kufanya ni kutembelea kituo cha afya ya uzazi au (VCT). Hapa utapata ushauri – Kisha kama uko tayari kuendelea na uchunguzi huo, Utatoa damu ambayo inapelekwa kufanyiwa uchunguzi, kuona kama ina virusi. Matokeo hayachukui muda mrefu kutolewa, na waweza kuyasubiri.

Tayo cartoon
TAYO
Pengine itahijitaji uchunguzi kama mara mbili tatu hivi kubainisha kwa yakini iwapo mtu ameambukizwa au la. Hii ni kwa sababu inachukua kipindi cha kama miezi mitatu kuanzia siku ya kuambukizwa kwa virusi kuweza kuonekana wakati wa uchunguzi.

Pengine swala la kusubiri kwa mda huu ndiyo sehemu ngumu zaidi ya utaratibu wa kuchunguza virusi vya ukimwi, lakini kusubiri kuna maanisha kwamba utakuwa na uhakika wa matokeo.

Huduma za uchunguzi wa virusi vya ukimwi zinapatikana kwa urahisi. Wasiliana na daktari wako au tembelea tu kituo cha huduma za afya ya uzazi kwa vijana kama vile VCT. Kama una wasi wasi kuhusu kuhifadhiwa kwa siri zako, usiwe na hofu.

Katika kliniki nyingi kuna utaratibu kabambe wa kuhifandhi siri za wateja. Haya yote utafahamishwa na mshauri wako, ikiwemo ni vipi uchunzguzi huo unafanywa, vipi utapokea majibu na hata kupata ushauri zaidi wa jinsi ya kuishi na virusi iwapo kwa bahati mbaya itabainika kuwa tayari umeambukiza.

Kumbuka Kama umefanya mapenzi bila kinga, ama unafikiria kuna uwezekano wowote kwamba umeambukizwa virusi vya HIV ni vyema kufanyiwa uchunguzi huo.

Usiendelee kuhatarisha maisha yako na ya wengine – Uamzi wa kwenda kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya HIV unaweza kuwa mgumu, lakini ni busara kwako na kwa wengine kutafuta usaidizi na ushauri wa kitaalam mapema iwezekanavyo.

Jinsi ya kuepuka maambukizi ya HIV.
  • Usijihusishe na ngono isiyo salama. Tumia kinga kila mara unapofanya ngono. Ukweli ni kwamba hakuna tendo la ngono lililosalama kwa asilimia 100. Kutumia kinga ni kupunguza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV ukimwi, na magonjwa mengine ya zinaa. Kwa hivyo daima tumia kondom na uyafuate maagizo kikamilifu.
  • Usichangie sindano.
  •  
Jinsi mtu anavyoambukizwa virusi vya HIV.
Mtu huambukiwa virusi vya HIV kama kirusi cha HIV kitaingia kwenye mishipa yake ya damu, wakati majimaji yake ya mwili yatatangamana na yae ya mtu ambae tayari ameambukizwa.

Virusi vya HIV hupatikana kwa wingi kweye majimaji haya ya mwili wa mtu ambae tayari ameambukizwa.
  • Damu
  • Manii/ Shahawa
  • Majimaji ya ukeni, ikiwa ni pamoja na hedhi
  • Maziwa ya matiti
Kwa kawaida majimaji mwengineyo ya mtu aliyeambukizwa kama mate, jasho na mkojo huwa hayana idadi kubwa ya virusi, kutosha kumwambukiza mwingine.

Ndio sababu maambukizo ya virusi vya HIV hutokea zaidi kupitia ngono na aliyeambuzwa, kuongezwa damu iliyo na virusi, mama aliyeathirika kumnyonyesha mtoto, au kuchangia sindano na mwathirika nk. Na hali yenginezo kama hizo.

Wakati wa kufanya ngono virusi hivyo huweza kupenya na kumwingia mtu mwengine kupitia maeneo nyororo ya ukeni, uumeni, sehemu ya kupitisha haja ndogo na hata njia ya kupitisha haja kubwa kwa wale wanaotumia njia hiyo kufanya ngono.

Kufanya mapenzi katika hali ya kuwa sehemu za siri ni kavu huongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV pamoja na magonjwa mengine ya zinaa.

Ngono kavu
Hii ni katika ile hali ya kufanya ngono ilhali eneo la ukeni halina ule unyevu nyevu wake wa kawaida. Hali hii huongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV na pia magonjwa mengine ya zinaa. Baadhi ya watu, wana itikadi kwamba wanawake wenye unyevu unvyevu mwingi ukeni, wanapenda mno kufanya ngono hivyo basi ni mzinzi.

Ukweli ni kwamba wanawake kimaumbile hutoa majimaji hayo wakati miili yao inajitayarisha kufanya mapenzi. 

“Kuwa tayari kwa mapenzi” hakumaanishi kwamba uko tayari kufanya ngono na mtu yeyote tu! Na kama wanamke hayuko “tayari kufanya mapenzi”, na akaendelea na kufanya ngono kavu, (iwe kwa kulazimishwa au kwa hiari) husababisha maumivu makali kwa mwanamke, na kumsababishia pia kupujuka hali inayozidisha hatari ya kupata maambukizo.

Kuwa na Virusi vya HIV ilhali u-mja mzito
Hatari kwa mtoto wako
Imekadiriwa kwamba asilimia kati ya 25 na 45 ya wanawake wenye virusi vya ukimwi, na wamepata pia mimba, wanaweza kuwaambukiza watoto wao ambao hawajazaliwa. Kwa hivyo wanahitaji ushauri wa kitaalam na dawa spesheli ili kupunguza hatari kuwaambukiza watoto wao.

Virusi vya ukimwi vinaweza kusambazwa kutoka kwa mama mja mzito aliyeambukizwa, hadi kwa mtoto tumboni kwa njia tatu:
  • Wakati mtoto yungali tumboni mwa mama, ambapo virusi vinaweza kusambaa kutoka kwa mama hadi kwenye nyumba ya uzazi.
  • Wakati wa kujifungua, ambapo mtoto anaweza kuingiwa na majimaji ya ukeni au majimaji mengine kutoka kwa mama.
  • Wakati wa kunyonyesha, ambapo virusi vinaweza kuambukizwa kupitia maziwa anayonyonya.
Uwezekano wa kumwambukiza mtoto, wakati wa kujifungua ni mkubwa zaidi kama mama ana ujazo mkubwa wa virusi mwilini mwake na kinga yake tayari ni dhaifu.

Kabla ya wanamke aliyeambukizwa kupewa usaidizi wowote wa kimatibabu kwanza atafanyiwa uchunguzi wa damu kuona kima cha virusi ndani ya mwili na hali yake ya kinga kwa ujumla.

Kama kinga yake itakuwa thabiti na idadi ya virusi ni ndogo mwilini, huenda hatahitaji dawa mpaka kipindi cha mwisho mwisho cha uja uzito yaani baada ya wiki ya 24.

Lakini kama ujazo wa virusi ni mkubwa na kinga mwili ni dhaifu, huenda italazimu kutumia madawa spesheli ya kupunguza makali ya ukimwi, mapema ili kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto.

Hatari ya kumwambukiza mtoto virusi vya ukimwi inaweza kupunguzwa hadi kufikia kati ya asilimia, moja na asilimia mbili tu kama hatua zifuatazo zitazingatiwa.

Kupata matibabu ya kupambana na virusi vya Ukimwi
  • Kwa sasa hivi hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba kutumia madawa ya kupambana na makali ya virusi vya HIV (ARV), kunamletea madhara mama na mtoto ambaye hajazaliwa.
  • Madawa ya kupambana na virusi vya ukimwi haswa AZT, yamethibitishwa kupunguza kwa asilimia kubwa, hatari ya mama kumwambukiza virusi hivyo mtoto wake wakati wa uja uzito .
  • Kama tayari unatumia madawa hayo ya ARV, kisha ukagundua kuwa u-mja mzito, mfahamishe daktari wako haraka iwezekanavyo. Kwa kawaida huwa ni vyema kuendelea na matibabu, lakini huenda ikakulazimu kubadilisha madawa. Kwa vyovyote vile, usisite kutumia madawa hayo bila ya ushauri na daktari.
  • Siku hizi inawezekana kupewa madawa ya ARV, ili kukabiliana na virusi vya ukimwi, kupitia kwenye mishipa ya damu wakati wa uchungu wa kujifungua. Inaaminika kwamba kufanya hivyo kunapunguza hatari ya kumwambukiza mtoto virusi hivyo wakati wa harakati za uchungu wa kujifungua.
  • Pia, ni kawaida mtoto wako kupewa madawa ya kupambana na virusi vya ukimwi ili kuzuia uwezekano wowote wa kuambukizwa.
Kuzaa kwa njia ya upasuaji
  • Ukichagua njia ya kuzaa kupitia upasuaji, yaani caesarean section kwa kimombo, kwaweza kupunguza kwa asilimia kubwa, hatari ya mama kumwambukiza mtoto wake virusi vya ukimwi.
  • Utaratibu huu humkinga mtoto asiingiwe na damu ama majimaji mengine ya mwilini na pia inamaanisha kwamba hutapata maumivu yanayoandamana na uchungu wa mda mrefu wa uzazi, hali inayoaminika kuchangia uwezekano wa mama kumwambukiza mtoto.
Kutonyonyesha
  • Inapendekezwa kwamba wanawake wenye virusi vya ukimwi wasiwanyonyeshe watoto wao bali watumie maziwa mbadala, kama ya ngo’mbe au maziwa maalum ya unga kwa watoto.
  • Hilo pekee linasadikiwa kupunguza hatari ya mtoto kuambukizwa virusi kwa kati ya asilimia 10 hadi 20.

Alhamisi, 28 Mei 2015

UNAJUA MUDA MZURI WA KULALA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1sTHo_6lwiixQLWGgDLHghOjx-j0e1xT-Rxx5ZEBBTot4NgiVDqj8M-xOeTgc5eZxwjYpKZgoLWEqaJqE3ymy7YRIcWBGbx_73BmpcrcVLAyMmZ9dqc_SAYVnjmcoCzvDDgx0664rrbSe/s640/19.jpg

Ni salama kusema kwamba kupumzika ina hatimaye kuota! Siku hizi ni nyepesi,  

Ndani ya masaa machache ndani ya masaa ishirini na nne unaweza kupata mawazo mapya na fikra mpya kuhusu maisha, maendeleo na hata kupata nguvu mpya tena ya kujipanga kwaa jili ya kukabiliana na mambo yanayo kusonga Lakini akili zetu na miili mara nyingi imekuwa haikubaliani na hali harisi kutokana na uchovu

Hata ivyo kutenga muda wa mazoezi nijambo la muhimu sana na baada ya mazoezi inatakiwa upate muda mzuri wa mapumziko  


Usingizi unatakiwa kueshimiwa kwamujibu wa , Dautovich anasema ufunguo wa kulinda usingizi wako ubora ni kuweka heshima (na heshima ya usingizi wako mara kwa mara) kama iwezekanavyo.

Msisimko kusababisha  wewe kusahau kuingia  kulala kila usiku masaa nane, baada ya kula ili kuongeza ufahamu wako na tabia yako pia .  

Kutoka vifaa vya umeme high-tech kwa kalamu-na-karatasi journaling, na kufanya juhudi fahamu kufuatilia wakati kufunga chini wakati wa usiku na kuamka asubuhi inaweza kukusaidia kuelewa uhusiano kati ya usingizi wako, mazingira yako na tabia yako, na vile vigezo wanaonekana kuleta usingizi bora.