Jumanne, 26 Agosti 2014

WAZAZI WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA ELIMU



Wazazi na walezi wametakiwa kuwekeza katika elimu ya watoto kwa kuwa kufanya hivyo ndiyo bima pekee bora kwa maisha yao ya baadaye na Taifa kwa jumla. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Naweza Kufikiri, Naweza Kuzungumza.

 Mashindano hayo yanashirikisha wanafunzi zaidi ya 100 kutoka shule 37 za sekondari wilayani Mufindi na lengo la kuanzishwa ni kuwajengea wanafunzi uwezo wa kufikiri.Mhagama alisema wakati umefika kwa Watanzania kuwekeza katika elimu ili kulikomboa Taifa kutoka katika umaskini, ujinga na maradhi.

 

Jumamosi, 23 Agosti 2014

BEN POL: SIHITAJI KWENDA NJE YA NCHI


 

Ben Paul 


Wakati wasanii wengine wakifanya juhudi kuhakikisha wanasafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutengeneza video za nyimbo zao,, mwimbaji mwenye sauti ya kuvutia, Bernard Paul maarufu ‘Ben Pol’ amesema kuwa hana mpango wa kutengeneza video nje ya Tanzania.

 

Ben Pol amesema licha ya video zake nyingi kuwa amezifanyia hapa nchini, lakini zimefanikiwa kuonyeshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni Afrika Kusini na Afrika Mashariki kwa jumla.

 

“Iwapo nitataka kutengeneza video kali ya kimataifa, nitamchukua mwongozaji kutoka nje na kumleta hapa Tanzania,” hivi ndivyo anavyosema.

 

Anasema kuwa ndani ya Tanzania kuna vivutio vingi anavyoamini akimchukua mwongozaji mwenye vifaa vya kutosha vya kimataifa, ataweza kutengeneza video yenye ubora.

 

“Unapomchukua mwongozaji kutoka nje na kumleta hapa, bila shaka itampa umakini mkubwa hata yeye mwenyewe, hivyo kufanya mambo makubwa zaidi ya afanyavyo akiwa huko. Hapa kwetu tuna vivutio vingi , maeneo yanayovutia kuna Lushoto, Arusha, Zanzibar, Bagamoyo na mengine yanayoweza kutumika kwa shughuli hii na ukaushangaza ulimwengu,” anasema Ben Pol.

 

Anasema kuwa bado anahisi anao wajibu wa kuutangaza utalii wa ndani kupitia kazi yake ya muziki.

 

“Nina wajibu na jukumu la kuwa balozi mzuri nyumbani kwetu. Najua labda watu wa nje wangependa kuona vitu vya nyumbani, ninapojitangaza kwamba mimi ni mwanamuziki kutoka Tanzania, hata kwenye kazi zangu waone mazingira ya nchi yangu,” anasema.

 

Je, hiyo ni sababu pekee ya uamuzi wake kufanyia kazi zake Bongo?

 

Ben Pol anaeleza kuwa, anapoona kazi zake zinatumika na kuombwa na watu wengi waishio nje ya nchi, hufarijika kwani inaonyesha inaeleweka.

 

“Najua kazi yangu inaeleweka, kwa watu wanaoijua lugha ninayoimba, hata kwa wale ambao Kiswahili kwao ni mtihani. Napokea pongezi nyingi, mfano wimbo wa ‘Jikubali’ ni kati ya kazi zangu zilizonipa umaarufu mkubwa nje ya nchi na ndiyo wimbo uliopigwa zaidi nje kuliko kazi zangu zote,” anasema Ben Pol.

 

Kuhusu usimamizi wa kazi zake Ben Pol anasema kuwa kwa sasa kuna mtu wa karibu anayemsaidia katika suala hilo. Anamtaja kuwa ni mshirika wake wa karibu na wanasaidiana katika kazi za muziki, lakini hana meneja.

 

Anabainisha kuwa kuna faida kubwa kwa msanii kuwa na usimamizi, lakini akasema bado kuna uhaba wa mameneja wa kazi za wasanii na kwamba kwa walipo sasa, wengi hawana ufahamu wa kazi zao.

Jumatano, 29 Januari 2014

HARAKATI ZA KUJIOKOA MORO



 Baadhi ya watu wakibeba chakula cha misaada kutoka kwa wasamaria wema. Picha na Juma Mtanda

MASHABIKI WANAO NG'ARA



Mashabiki watoto (walio mstari wa mbele) wakiishangilia timu yao ya Ashanti United wakati mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha na Michael Matemanga