Jumanne, 9 Juni 2015

SIKIA ALICHO KISEMA NISHER BYBEE "Mijitu mingine mnakua ..." AMBAE NI >>> Director / Producer / Recording Artist / Musician / Actor / Recording Engineer



Kula vizuri, Vaa Pendeza, Ishi unavyo taka (usivunje sheria za nchi), Nunua unachopenda, Mwisho wa siku Furahi!!! Hayo ndo maisha... Mijitu mingine mnakua na Streeeeeeessssss kisa mwenzako Anaishi vizuri, hayo sio maisha, hizo ni Njaa!

Jumapili, 7 Juni 2015

FANYA HII VII ILI KUZUIA KUHARISHA UNAPOKUWA SAFARINI>>> Maji yanaweza kukufanya ukawa mgonjwa pia*** http://baragumuhabari.blogspot.com/

Image result for kuharisha
 Kwa nini uharishe wakati ukiwa safirini?
Kuna maambukizo mengi watu hupata wakati wanaposafiri na ambayo huleta kuharisha. Mengi ya haya maambukizo hayadhuru watu wanaoishi katika sehemu hizo ambazo wewe unasafiri kwani wao huenda walishaugua kabla (na sasa wamejenga kinga). Watu pia huharisha wakati wanaposafiri kutokana na uchovu wa safari na kubadilisha chakula.


Nitajuaje kama kuharisha kwangu ni maambukizo au ni kutokana na sababu nyingine?
Ni vigumu kusema tofauti yake. Kama unaenda choo laini 2-3 kwa kutwa na bila dalili nyingine zozote, kuharisha kwako sana sana huenda haukuambukizwa na vimelea vibaya. Maambukizi haya yatafuatwa na kupata choo cha maji maji mara nyingi. Dalili nyingine ni pamoja na kuharisha damu, homa, maumivu ya tumbo na kichefu chefu.

Nitazuiaje kuharisha?
Kitu cha maana kabisa na rahisi ili kuzuia kuharisha ni kuosha mikono mara kwa mara. Kufanya hivi ni muhimu sana haswa kabla ya kula chakula, pia mara nyingi kuosha mikono mara kwa mara ni vizuri. Kwa kuwa sabuni na maji sio ghali na hupatikana kila mara, kuna vitambaa vilivyolowekwa katika dawa za kuulia wadudu (hufanya kazi vizuri sana) huwa ni rahisi zaidi kutumia wakati ambapo sabuni na maji havikupatikana. Vitambaa hivi hupatikana katika maduka mengi ya dawa, hata ya vyakula au stoo za vitu mchanganyiko huko Umarekani, vichukue vitambaa hivi uendapo safari. Kama hujui jinsi ya kuvipata, mwulize daktari au muuguzi wako.
 
Vyakula vingine ni salama zaidi. Chakula chochote au kinywaji ambacho ni cha moto sana wakati kinapoandaliwa ni salama. Mikate, pipi pia ni salama.

Vyakula ambavyo vina hatari ya kuleta madhara na kukufanya uwe mgonjwa ni kama mboga mboga mbichi, saladi na vinginevyo vibichi au vilivyopikwa na kuiva nusu kama vile samaki na nyama. Kama utaosha mikono yako na kutumia kisu kisafi kumenya na kukata tunda, kwa kawaida ni salama. Epuka matunda ambayo hayana kumenywa kama vile matunda damu. Vyakula vya maziwa kama vile maziwa na jibini si salama labda kama vimesindikwa kwa ufundi (kuchemsha kwa mvuke). Unaweza kutengeneza maziwa salama kwa kuyachemsha mpaka kuchemka na kuyaacha yapoe. Maziwa ya pakiti (irradiated milk) ni salama kwa kunywa.
 
Maji yanaweza kukufanya ukawa mgonjwa pia. Kama maziwa, ukichemsha maji yako yatakuwa safi na salama kwa kunywa. Maji yauzwayo, yaliyohifadhiwa kwenye chupa pia kwa kawaida ni salama kwa kunywa. Vinywaji vilivyosindikwa kwenye chupa (vyenye kutoa vipele vya hewa kama vile soda) pia ni salama kwa kunywa. Hewa ya carbon inayotiwa katika vinywaji vilivyosindikwa pia huua vimelea kwa kipindi cha masaa manne, hata hivyo kutia hewa hii katika bomba la maji haifanyi maji yake kuwa salama kunywa kwani maji yaliyochanganywa hayakuwa yamechemshwa. Ni lazima uepuke kutumia vibonge vya barafu labda viwe vimetengenezwa na maji safi na pia wakati wa kupiga mswaki utumie maji safi na salama.
Itakusaidia zaidi endapo utafanikiwa kuepuka vyakula vya aina fulani kwa kuwa tumbo lako halikuvizoea japo vilizoeleka zamani.
 
Nifanye nini kama nitaharisha?
Kuna aina mbili za dawa za kuzuia kuharisha kwa wasafiri. Ya kwanza ni zile dawa za kupunguza kasi ya kuharisha lakini hazitibu maambukizo yaliyoleta kuharisha. Dawa hizi zinasaidia kupunguza dalili za ugonjwa. Dawa zinazotumika sana zinaitwa loperamide (“Imodium”) na Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”), ambazo zote zinapatikana maduka yote ya dawa bila ya agizo la daktari.
Dawa hizi zisitumiwe na watoto wadogo.
Pia, kuna (antibiotics) dawa zinazoua vimelea vibaya ndipo hutibu ugonjwa. Kwa kuzitumia dawa hizi huweza kupunguza idadi ya siku za ugonjwa.
 
Wakati unapoharisha maji maji ni lazima utumie (antibiotic) dawa za kuulia vimelea vya ugonjwa ambazo daktari au muuguzi wako atakupa uchukue safarini. Unaweza pia kutumia loperamidend Bismuth subsalicylate kuzia kuharisha mpaka dawa ya kuulia vimelea vibaya ifanye kazi. Kama uko
taabani, una homa au unaona damu katika choo chako, ni lazima utumie dawa ya kuulia vimelea (antibiotic) na SIO ile ya leperamide au Bismuth subsalicylate.

VITU VYA KUKUMBUKA WAKATI WA KUSAFIRI
OSHA MIKONO, Na kama Huwezi kuosha mikono vya kutosha, hasa kabla ya kula  Basi (tumia vile vitambaa vilivyowekwa dawa ya kuulia vimelea vibaya kama Purell au Aavanguard kama ni rahisi zaidi kutumia) wengine huita sanitizer.

EPUKA VYAKULA HIVI.
Vibichi, au nyama, samaki, isiyoiva vizuri, maziwa ambayo hayajachemshwa au jibini, majani ya mboga mboga. Matunda ni lazima yaandaliwe kwa njia ya usafi, mahindi yakuchemsha na vyakula kama hivyo.

MAJI NA MAZIWA
Vinaweza kufanywa kuwa safi na salama kunywa kwa kuchemshwa na kuacha chini vipoe.
 Maji yanayouzwa katika chupa kwa kawaida ni salama.
Kama umeenda choo laini mara moja au mbili kwa siku tumia dawa ya  kukusaidia katika dalili hizi, lakini choo cha maji maji kabisa haswa kuchanganyika na damu, maumivu na homa, tumia dawa ile ya kuulia vimelea vibaya (antibiotic).

DAWA ZA KUZUIA KUHARISHA
Wakati uonapo dalili:
Loperamide (“Imodium”)
Matumizi: Kunywa  vidonge viwili kwa kuanzia, kisha kunywa kidonge kimoja kila  upatapo choo (usinywe zaidi ya 8 katika masaa 24). Usiwape watoto wachanga, wadogo au ukiwa mja mzito.
 
Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”)
Matumizi; Kama ni vidonge meza vidonge viwili kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha  kupungue. Hata hivyo usinywe vidonge zaidi ya 16 katika masaa 24. Kama unakunywa vitu vya maji maji, kunywa vijiko vya chai 6 (30 mls) kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha kupungue. Usinywe vidonge zaidi ya 8 katika masaa 24. Usiwape watoto wachanga na watoto wadogo.

kutibu Maambukizo
Antibiotic:
Daktari au muuguzi wako atakupa dawa ya antibiotic kusafiri nayo unywe  ukipatwa na kuharisha kubaya. Hakikisha kuwa unaelewa jinsi ya kunywa dawa hizi kabla ya kuondoka katika ofisi ya daktari au muuguzi. Majina ya dawa za antibiotic zinazotumika na kujulikana sana ni kama Azithromycin (Zithromax), Ciproflaxacin, Levofloxacin (Levoquin) na Fifaxaamin Na pia utaandikiwa dawa kwa mujibu wa daktari.

Ijumaa, 5 Juni 2015

CHEKI HAPA ALICHO KISEMA A.Y KUHUSU MKOA WA NJOMBE... MWANA FA NAE KAJIPANGA KUFANYA ANACHOKIJUA

Nani anakuja leo kwenye show yangu pale Club Vibe, Mbeya na kesho Jumamosi pale Club Vegas, Njombe? Njoo mtu wangu tukutane, tujuane na tupige mapicha kibao ya kuwalingishia washkaji hapa Facebook na Instagram!

Jumatano, 3 Juni 2015

HUJAWAHI JIULIZA KWA NINI WATOTO WA MJINI DAR WANAONGEA KICHIZI NA WANAJIAMINI SOMA HAPA UTAJIFUNZA KITU>>> Hii inatakiwa kuigwa na watu wa mikoani



Image result for picha ya nazi











Namna ya kufanya:

 Utahitaji;

1.  Nazi. Yaweza kuwa nazi, mafuta ya nazi, tui la nazi, dafu n.k.

 Image result for picha ya nazi
2.  Chai mbichi isiyokaushwa.

3.  Vyakula - mchanganyiko wa nafaka.



Nazi imewahi kuthibitishwa kuwa na vitu muhimu vinavyoua virusi. Lauric Acid ndiyo acid pekee kwa kuua virusi ambayo inapatikana toka katika nazi na pengine ni toka kwenye maziwa ya mamaake binadamu tu duniani kote.

 Je, Ni kweli Nazi inarutubisha afya?
Acid hii ndiyo kitu pekee chenye uwezo wa kuua virusi na ni rahisi kugundua hilo kama utakuwa mtu mwenye kumbukumbu basi nakupa Uthibitisho katika maeneo matatu.

 Image result for picha ya nazi

Linganisha afya mbovu za awali za watu waliohamia Dar Es Salaam kama vile wasichana wa kazi za ndani, vijana wanaokuja kusoma au kuutafuta maisha n.k. wakitokea sehemu zisipopatikana nazi. 

 Utamkuta mtu anakuwa hajiamini, haongei sana, mwoga, ngozi yake imejikunja-kunja, miguu imepasuka na pengine hata kitambi cha kwashakoo ni kawaida kwao. 

Halafu angalia afya zao pale walipokula vyakula vilivyoungwa nazi kwa muda mfupi tu kama miezi mitatu tu wakiwa hapa Dar Es Salaam. 

Image result for picha ya nazi

Utagundua kuwa afya zao zilibadilika sana.Wananenepa, Mipasuko kwenye miguu inaondoka, Ngozi zinakuwa nyororo, kwashakoo inaondoka, wanakuwa sio waoga tena, wanaongea sana tena kwa kujiamini na kwa kusema yote ni kuwa wanachangamka kiafya.

 Image result for picha ya nazi

 Kwa wale tuliosoma “Old schools” mtakumbuka tulisoma vitabu vingi vikiwemo Alfu lela Ulela ambavyo vilijumuisha Safari saba za Sindbad Baharia.

 Katika safari zake aliwahi kutekwa akiwa na wenzie saba baada ya chombo chao kugonga mwamba na kuvunjika. 

Watekaji waliwafungia ndani na kuwalisha “wali ulioungwa nazi”  ili wanenepe kisha wawachinje! Sindbad kwa kujua hilo hakula kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi wenzie walinenepa sana na walichinjwa wakaliwa! Yeye alikuwa akikonda siku baada ya siku na kuwafanya maharamia hao kumfungulia atembee tembee awe huru ili aimarike kiafya na ndipo alipopata mwanya wa kutoroka….

Uthibitisho wa mwisho ni pale mtoto mchanga anapofiwa na mama yake basi huwa anaikosa lauric acid toka ziwa la mama na afya yake nadhani wote mmeshuhudia inavyoathirika. 

Kifupi ni kuwa anatakiwa pamoja na maziwa ya wanyama anayolishwa inatakiwa apate walau kijiko kimoja cha tui la nazi kila siku ili kuilinda afya yake isiporomoke.

Hivyo kama wewe ni muathirika wa maradhi ya aina yoyote, basi tumia dawa za hospitali, halafu ili kuthibitisha hili jaribu kula vyakula vilivyoungwa nazi kwa kiasi kikubwa, au chakula kilichokaangwa kwa mafuta ya nazi, au jenga mazoea ya kutafuna nazi mbichi na pengine ni vizuri zaidi ukaacha tabia ya kunywa soda na kuanza kunywa maji ya madafu pale unaposikia kiu.

Je Nazi yoyote inatibu?
Kama kawaida ya uhusiano wa mmea na udongo ulivyo, zipo nazi ambazo ukizipeleka katika maabara utazikuta zina kiwango kikubwa cha lauric acid au ukakuta lauric acid ipo kidogo au pengine ukakuta nazi haina kabisa lauric acid kwa vile udongo ulipooteshwa nazi kuna kemikali ambazo zinasababisha udongo huo kuwa sio sahihi kuzalisha acid hiyo katika nazi. 
  
Pia mpaka sasa yapo makampuni ya kusindika nazi ambayo yanakamua nazi zenye lauric acid ya kutosha na kuuza kama dawa. 

Nazi hizo zimeingizwa nchini na ninazitumia kutoa tiba kwa waathirika na hakika zinapunguza idadi ya watu wenye afya mbovu. 

Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zilizowafikia wawekezaji wa ndani hasa katika sekta ya afya ambao ningeweza kushirikiana nao kuitafiti bidhaa hii nchini watu wale na wapone.

Je, Nazi zinapatikana?
Upande wa pili wa shilingi una sura ya nazi kuwa bidhaa ya wenye nazo tu mara baada ya habari hii kuenea. 

Sasa Vile vile ni vema kwa wizara za kilimo na chakula pamoja na wizara ya afya kukaa chini na kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto hii ya kupungua kwa nazi masokoni pamoja na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo ambayo inaweza kufikia shilingi elfu tatu kwa nazi moja endapo theluthi moja tu ya watanzania wataamua kuitumia nazi kama dawa ya kurutubisha afya zao.

Wakati naendelea kukuletea habari hii, ni vema ukaituma email hii kwa watu ishirini au wote katika address book yako ili tupunguze idadi ya watu wenye matatizo ya kiafya. Tusifiche tiba maana kuwa na taifa lenye wagonjwa ni UMASIKINI. Tafadhali tuma sasa.