Jumatatu, 11 Februari 2019

R. KELLY NI MOTO WAKUOTEA MBALI NCHINI UJERUMANI.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari za burudani wa Veltra, umeripoti kuwa R. Kelly atatumbuiza mjini Ludwigsburg nchini Ujerumani mwezi April 12, 2019. Hii ni baada ya kubadilisha ukumbi mara mbili kutokana na uhitaji wa tiketi kuongezeka.
Awali R. Kelly alipangiwa kutumbuiza katika ukumbi wa MHP Arena unaochukua watu 7,200, uliopo mjini humo lakini baadae mapromota wakabadilisha ukumbi wa show hiyo na sasa itafanyika katika ukumbi wa 
Ratiopharm Arena unaochukua watu 9,000 .
Image result for UKUMBI ULIO JAZA

TUZO ZA GRAMMY ZA PAMBA ZA TIKISA ALFAJIRI YA LEO.

Kwa mara ya 61 tuzo hizi kufanyika nchini Marekani, kuna orodha kubwa ya wasanii walioshinda tuzo za Grammy na kuna wasanii waliokuwa kivutia katika tuzo hizo. Drake na Cardi B ndio walikuwa gumzo zaidi huku Cardi B akishinda tuzo na Drake akiondoka na tuzo lakini walikuwepo wengi walioshinda tuzo tofauti tofauti.

Image result for drake

Alhamisi, 21 Juni 2018

WANAKIJIJI WAUZA FIGO KWA SABABU YA HALI DUNI KIUCHUMI



kuna hii ya kuifahamu kuhusu Kijiji cha Hokse nchini Nepal kimebatizwa jina jipya la ‘Kidney Village’ baada ya Watu karibia wote wanaoishi kwenye kijiji hicho kuwa wameuza Figo zao.
 
Inadaiwa kuwa Wakazi wa Kijiji hicho hali zao za kiuchumi ni duni sana kitu kinachowasukuma kuingia katika biashara ya kuuza Figo zao ili wapate fedha za kujikimu mahitaji yao.

Mkazi mmoja aliyetambulika kwa jina la Geeta mwenye miaka 37 alisema kuwa yeye na Mume wake walisafiri mpaka kwenye Hospitali moja huko nchini India ili kutolewa Figo zao na kulipwa  zaidi ya shilingi Milioni 3 za Kitanzania.

Aidha familia hiyo ilitumia fedha hizo kununua kiwanja na kujenga nyumba yao na isivyo bahati nyumba hiyo iliangushwa na tetemeko la ardhi lililotokea kijijini hapo.

Kwa upande mwingine madalali wanaofanya biashara hiyo ya figo wametajwa kuzunguka sana katika kijiji hicho na kuwashawishi Wanakijiji hao kuuza Figo zao.

Jumatano, 9 Mei 2018

MVUA KUBWA ITAKUJA KWA SIKU TANO MFULULIZO #TMA

See the source image
Mvua kubwa yatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Utabiri huo umetolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini (TMA), ambao umeeleza kuwa kiwango hicho cha mvua kilitarajiwa kuanza jana usiku.

Kwa mujibu wa utabiri huo kiwango cha mvua hiyo kitaendelea kwa siku tano hasa wanaoishi mabondeni, wametakiwa kuchukua tahadhari.

TMA imeeleza kwamba athari zinazoweza kutokea ni mafuriko ambayo yatasababisha msongamano wa magari na watu hali itakayochelewesha usafiri na usafishwaji maeneno ya mjini.

Aidha kwa siku ya jana asubuhi kulikuwa na wingu zito lililoashirijia ujio wa mvua kubwa, lakini haikunyesha mvua hiyo kama ilivyotarajiwa huku asubuhi ya leo majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam imenyesha mvua ambayo imedumu kwa kipindi kifupi.

Jumanne, 8 Mei 2018

CHUI ALIYEMLA MTOTO WA MIAKA MITATU NCHINI UGANDA ATAFUTWA

See the source image

Maafisa wa nyama pori nchini Uganda bado wanamsaka Chui aliyemla mtoto wa miaka mitatu

8.5.218 KUNAUWEZEKANO WA KUFUTWA KWA KESI YA MKURUGENZI WA SHULE YA LUCK VICENT

Mahakama ya Wilaya ya Arumeru imetishia kuifuta kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vicent na wenzake kwa sababu ya upande wa mashtaka kuomba kesi hiyo iahirishwe mara kwa mara.
Hayo yamesemwa na Hakimu wa mahakama hiyo, Desderi Kamugisha baada ya wakili wa serikali, Alice Mtenga kuomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine ili waifanyie mabadiliko hati ya mashtaka.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Wakili wa utetezi, Method Kimomogolo alikubaliana na hoja za wakili wa serikali, kwamba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Hakimu Kamugisha alikubaliana na ombi la ahirisho la kesi hiyo, huku akiuonya upande wa mashtaka kwamba kama haujajipanga vizuri kuhusu kesi hiyo anaweza kuifuta kwa sababu inaahirishwa mara kwa mara.
Baada ya kusema hayo aliahirisha kesi hiyo hadi May 8, 2018 kwa ajili ya kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.

8.5.2018 NCHINI HAWAII WANANCHI WAMEONDOLEWA MAJUMBANI MWAO



a fire in a field: Lava flows across a yard in the Leilani Estates neighborhood of Pahoa, Hawaii on May 6, 2018.
Watu zaidi ya 1700 wameondolewa katika nyumba zao katika eneo Kilauea nchini Hawaii kutokana na tope la volkano.
Wakazi wa eneo ambalo limekumbwa na volkano wameondolewa wakihofiwa kudhurika kutokana na moshi wa tope la volkano na kupelekwa katika eneo salama.

Tope hilo la volkano linatoa moshi ambao wanasayansi wamesema kuwa ni hatari kwa maisha ya binadamu.